KWANINI HAITAKIWI KUOA MWANAMKE ALIEKUZIDI UMRI



Habari za muda huu mdau na mfuatiliaji wa makala mbalimbali zinazokujia kupitia katika blog yetu, naomba nichukue nafasi hii kukuarika rasmi mahala hapa ambapo siku ya leo tutangalia athari za kuwa na mahusiano na mwanamke aliyekuzidi umri.
Katika jamii zetu za kiafrika suala la mwanaume kumzidi umri  mwanamke katika sekta ya mahusiano limekuwa ni suala la kawaida sana, lakini pindi inavyotokea kinyume chake watu wengi hubaki vinywa wazi huku watu wengi wakishangaa kuona mwanamke mwenye umri mkubwa akiolewa ni mwanaume mwenye umri mdogo.
Jambo hili  huendelea kuleta gumzo sana, hasa pale linapotokea katika jamii yetu, hii ni kwa sababu inaaminika ya kuwa mwanaume ndio nguzo ya mahusiano hivyo mwanaume anatakiwa kumzidi umri mkewe, inapotokea kinyume chake huwa kuna athari kubwa katika mahusiano hayo.
Zifuatazo ndizo athari za kuwa na mahusiano na mwanamke ambaye amekuzidi umri:
1. Kupelekeshwa. 
Unapokuwa na mahusiano na msichana ambaye amekuzidi umri basi jiandae kisaikolojia kupelekeshwa na msichana huyo, sikutishi ila nakwambia ukweli lengo la kuingia kwenye mahusiano ni kupata amani ya moyo,  hivyo unapoingia katika mahusiano ya kimapenzi na msichana aliyekuzidi umri ni lazima utakosa kitu hiki kwa sababu ukweli ambao upo wazi ni kwamba msichana anapokuzidi umri basi yeye ndiye anayegeuka kuwa kichwa cha mahusiano. Hivvyo kitu chochote asemacho aidha ni kizuri au kibaya anategemea utakifanya kitu hicho.
2. Kutokuwa na maaumuzi yako. 
Unapoingia katika mahusiano na msichana ambaye amekuzidi umri basi fahamu fika yeye ndiye ambaye atakuwa ni kiongozi wa maamuzi yako, Kama unataka kufanya jambo lolote la msingi ni kwamba huwezi kukurupuka na kuanza kufanya jambo hilo pasipo kumshikirikisha huyo b. mkubwa katika suala la kutoa maumuzi.
Hayo ni baadhi ya matokeo machache kati ya mengi ambayo utayapata pindi utapokuwa na mahusiano na msichana aliyekuzidi umri.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post