Nakupenda mke wangu ingawa sikujui jina wala unapoishi; sijui unafanya nini muda huu, ila najua uko unapitia pitia post humu mtandaoni, na hii post ulioiona huenda nimeandika kwa ajili yako...
Naomba nikwambie my lav, nakupenda mke wangu mpole, ingawa sijui jina lako wala kabila lako, wala umri wako, wala rangi yako.
Ila najua ni mwanamke mzuri, una moyo wa upendo wa kweli kwa mwanamme mmoja!! Najua wewe ni mwanamke mwema, ulielelewa katika maadili mema na wazee. Najua wewe sio mvivu, ni mtafutaji na una uchungu wa maisha. Ni mwanamke unaeheshimu mambo ya dini na una heshima na nidhamu.
Una mawazo mengi ya maendeleo ila shauku yako umpate mwanamme atakaye kupenda kweli ili mchakalike kwa pamoja mfikie maisha unayo yatamani.
Umeumizwa, umelizwa katika mapenzi na wanaume ambao hawakuumbwa kwa ajili yako na ambao hawakujua kabisa thamani yako. Umekuwa ukinitafuta ukijiuliza, yuko wapi yule mwanamme aliyeumbwa kwa ajili yangu ili niondokane na maumivu haya? Kuna wakati huwa unakata tamaa ya kunisubiri na unasema mbona ninachelewa kuja?
Usikate tamaa mke wangu; usikate tamaa malkia wangu; usikate tamaa my lav. Hata mimi huku nilikuwa nikikutafuta ili nikupate hata mimi sijui nitakupataje:
Nimekutafuta sana; sijafa moyo, nimeona nije nikutafute hadi huku Whatsap kwani naamini ingawa whatsap imejaa watu wa aina mbalimbali, wema na wabaya, huenda malkia wangu mwema umo humu...
Sitajali nitakutana nawe sehemu gani, kwa njia gani na muda gani; popote pale, ilimradi tu nikupate hatimae malkia wangu. Usiogope pengine hii post ndio mwanzo wa kujuana na wewe mke wangu mpenzi!!
Usiogope kucomment kwenye post hii, huenda ndio mimi tunatafutana! Nani ajuae, huenda leo tumekutana hatimae. Tutasahau maumivu yote tulioumizwa nyuma na watu ambao hawakuwa wetu.
Najua comment zitakuwa nyingi baby, wapo watakaonidharau, wapo watakaonicheka, wapo watakaosema "nakuombea kwa mungu utampata", kisha wataenda zao. Lakini comment yako nitajua tu, kwani itaakisi na kudhihirisha shauku yako na furaha yako ya kunipata hatimaye mwanaume wa ndoto ya maisha yako. Najua hutasita kuchukua namba yangu nitakayokuachia hapo chini.
Nakupenda baby wangu, nakupenda my lav wangu, nakupenda laaziz wangu; natamani leo ndo iwe mwanzo wa kukutana nawe my Forever.
Welcome my Queen!! My future wife!!!
Post a Comment