KWA WALIYO KWENYE NDOA TU, NAOMBA MSOME HAPA TAFADHALI


1. Kila mwanaume anahitaji mke ambaye atampa mawazo bora na yenye tija kwa mustakabali wa ustawi wa familia.
.
2. Kila Mwanaume anahitaji mke ambaye hatampandishia sauti, bali atamheshimu na kumsikiliza.
.
3. Kila Mwanaume anahitaji Mke ambaye ni mkimya, asieongea sana kama kasuku na kupayuka hovyo bila kuchagua maneno ya kuongea.
Yaani ambae hajiinui na kujifanya mshindani wa mumewe ndani ya nyumba.
.
4. Hakuna mwanaume anaependa mwanamke mwenye gubu, wivu uliopitiliza na anayetoa maelekezo ili mume ayafuate.
.
5. Kila mwanaume anahitaji mwanamke ambaye atamsikiliza na atakayemuamini. Hata kama jambo fulani hakubaliani nalo, hataonyesha mbele za watu, atalisema wawapo wawili tu.
.
6. Kila Mwanaume anahitaji mke ambaye ataamka asubuhi, atamuandalia Maji ya kuoga na Breakfast kabla ya kila mmoja kwenda kwenye mihangaiko yake pale inapobidi ila kama mke yuko busy sana haina shida mume atakunywa popote na kuridhika.
.
7. Kumpenda mke ndio msingi mkuu, nae mke atakutii mumewe. Ni ngumu mnoo kumtii mtu "asiyekupenda". Mungu alitupenda sisi kwanza ndiyo maana tunamtii.
.
MKE MWEMA HUFUNGUA KINYWA CHAKE KWA HEKIMA, NA SHERIA YA WEMA I KATIKA ULIMI WAKE NA SI YUKE ANAESHUPAZA SHINGO KWAMBA HAKI SAWA.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post