Wakati mmoja nilikua kwenye mahusiano ya mbali, nilishafikia kipindi katika maisha yangu ambacho sioni tena sababu ya kuchepuka. Nilikua na furaha na sikutaka kuiharibu. Rafiki zangu (wale wapya ambao walikua hwawanijui kabisa) walikua hawanioni nikiwa na mwanamke, uzuri najua kusoma watu na kila tukiongea waliniona kama nina matatizo (wanakua na vimaswalimaswali) walihisi labda huyu mtu ana matatizo sio mzima, mbona hana mwanamke, mbona stori nyingi tu, mbona hivi mbona vile? Walikua hawaniulizi lakini walikua wanajiuliza na kuulizana, huwa nilikua nawasoma usoni nacheka tu!
Kuna wanaume wengi wanaingia katika mtego huu, kudhani kua kuwa mwanaume ni lazima kuwa na wanawake 10. Kwamba kutongoza kila mwanamke anayepita mbele yako na kuonyesha marafiki zako kuwa ni kidume. Huu ni utoto wa sekondari na kidogo sana chuoni, lakini ukishakua mtu mzima unatakiwa kujua kuwa huna sababu ya kuchepuka ili uonekane kidume. Kuna mwanaume anaenda Baa anatafutiwa mwanamke na marafiki zake anachepuka na kupiga picha kuwatumia ili aonekane alipiga show!
Mfano wanaume wengi ambao wanajihisi kama wana matatizo ya nguvu za kiume, wale wakwenda goli moja la dakika mbili tatu ndiyo wanaongoza kwa kuchepuka. Si kwakua wanapenda bali kwakua wanaamini kuwa kila mtu anawaona kuwa hawana nguvu za kiume na si marijali, wanaamini kwakua na wanawake wengi na kuwaonyesha ndiyo wataonekana wanaume sana. Tena wengine unakuta wanaringishia michepuko yao haya kwa wake zao kuwaonyesha kua huko nnje napendwa na naweza!
Unakuta mtu kwa mkewe ni dakika mbili pumzi imekata lakini ana wanawake 200 kidogo, mapicha ya uchi ndiyo usiseme, anaviahidi vidada vya watu ndoa na anavipa simu vimtumie meseji mkewe na kumpigia ili kumrusha roho. Tuseme ukweli unamrusha roho mke wako kwa kipi, anakujua kila kitu, hizo dakika zako mbili anazijua unafikiri riho itaruka? Akiamua kulipoa kisasi si utakufa maana yeye atatafuta wa masaa mawili! Niseme tu kuwa, chepuka kwakua ni Malaya unapata raha na si kwakua unataka kila mtu ajue wewe ni mwanaume au kujionyesha, haisaidii chochote!
Unataka washikaji zako wakuone rijali ili nini? Una mpango wa kutembea nao au? Unahangaika na kila mwanamke, huna raha, wanawake wenyewe unaotongoza ni wale wa rahisi rahisi ambao hata kukataa ni shida lakini unajishaua! Halafu hujishtukii kweli, unatembea na mwanamke ambaye anaweza kupiga picha ya uchi na kumtumia mke wake na bado unajiona kuwa wamaana unamrusha roho mke wako! Tuseme kweli mwanaume unamrusha roho mke/mpenzi wako kana kwamba mnagombea bwana au?
Post a Comment