Kuna mambo katika usichana wako ...katika usingle wako usiwe nayo mpaka yakapitiliza .

..maana yakipitiliza hautaonekana tena kama ndani yako kuna ustaharabu.
Mambo hayo ni pamoja na:
KURINGA KUPITILIZA.
Hakuna anaekukataza kuringa ..By the way wewe ni mwanamke ringa .. LAKINI KURINGA KWAKO KUSIPITILIZE.. Utamkwaza hata yule aliye na nia njema kwako...hataona tena kuringa kwako bali ataona bado kuna utoto ndani yako..
Ataona bado haujawa tayari kuwa mwanamke.
Sijajua kwa sisi wanaume kama kuna alieoko hivi...Kama yupo mwanaume anaringa namna hii basi aundiwe tume ya uchunguzi ...maana sio bure... Kutakuwa na mkono wa mtu...
KUWA NA KIBURI KISICHOKUWA NA MBELE WALA NYUMA.
Hii imewakosesha wasichana wengi watu waliokuwa na nia njema kwao na kujikuta wameangukia kwenye mikono mibaya ..mikono ya watu wanaokuona unakiburi lakini hata hawaangaiki na wewe maana wanajua wanapita hapo... wamepuzika kunywa maji ..then safari yao iendelee.
KUPENDA STAREHE KUPITA KIASI:
Hizi starehe za pombe na nyama ..kwamba usipozipata haujisikii poa ...uko tayari uuze utu wako lakini upate pombe nyama..
Hii ni mbaya sana kwako mwanamke ..maana mwanamke wa namna hii mara nyingi huangukia mikono ya wajanja ..hakuna mwanaume anaejielewa aje akuvamie ...wewe utakuwa unavamiwa na watu wa kukutoa out then ndani ya muda mfupi wanatembea na wewe kisha wanakuacha... Kumbuka kila mtu anapenda starehe ila isipitilize maana ikipitiliza saba itakufanya wanaume wakudharau.
Dayari Yangu
Image may contain: 1 person, standing, child, hat and outdoor


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post