KANUNI ZA UENDESHAJI WA UCHUMBA!



1: Ndoa ni MUNGU + MME +MKE, Ruhusu Mungu awe ndie kiini cha mahusiano Yenu, Zaburi 121:1
2: Mahusiano yenu yasiwe ya siri, watu wa karibu wafaham kama ndugu, jamaa na marafiki wawapendao, uchumba sio siri ( ili uwe uchumba lazima wazaz wenu wafaham kama hawafaham huo ni urafiki sio uchumba.
3: Shiriki huduma za kijamii, mchumba wako akishiriki huduma za jamii utajua Tabia yake nyingine akiwa na group la watu anajibuje anaongeaje na anavyoweza kusaidiana na kushirikiana nao vipi, Kuna wengine wana Tabia tofauti na Ile unayoijua, akiwa pamoja na wewe wawili yuko hivi akiwa na watu wengine yuko vile .....Mwanzo 24:17-19
4: Lindeni jina lenu lisichafuke, yaan msijiachie kwenye mahusiano ya kimapenzi kabla ya ndoa
5: kila mmoja amlinde mwenzake, yaan msiwashe moto wa mapenzi ambao hamuwezi kuuzima, ......Wimbo uliobora 8:7 na 2:7
6: Msikae mahali ambapo sio open place ili kuepusha uchochezi wa kufanya ngono, na kuleta maswali kwa watu wanao waona.
7: Si vibaya kumuonesha mwenzako hisia kama unampenda kweli maana upendo ni hisia, Ila iwepo mipaka na utaratibu, mwekeane speed limit, na kila mmoja aiheshim hiyo limit
8: fungueni mioyo mzungumze bila kufichana jambo lolote na muwe waz kila MTU kwa mwenzake, (kuwa huru na wazi mtazidi kufahamiana zaid)
9: Malizeni tofauti zenu kistarabu mara zinapojitokeza, sio kuachana (Waefeso 4:26)
10: Usikae na kinyongo moyoni ongeeni USO kwa uso , ongeen wakati hasira Kali imeisha na ktk mazingira tulivu.
11: Msiipuuze jambo lolote linalo leta tofauti zenu litafutien ufumbuzi
12: Chaguen wanandoa waliotangulia mnaowapenda na wao wanawapenda watakao Lea ndoa yenu (chagueni family yenye mfano wa kuigwa)
13: Jifunze lugha ya upendo kwa mwenzako ( TAFADHALI, POLE, ASANTE, NISAMEHE, NAKUPENDA)
14: Jambo asilolipenda mchumba wako liache Mara mojA, na lile analopenda likuze na uwe mbunifu kwalo zaidi
15: Ingia ktk mahusiano ya uchumba kama uko tayari kwa ndoa,
16: Mahusiano yanahitaji mawasiliano imara ili kuleta u karibu Zaid, mahusiano ya mbali (mkoa kwa mkoa, nchi na nchi yanahitaji mawasiliano ya mara kwa mara zaidi, Kuna Wale wategeaji kwamba ah kila Siku mimi ndie namtext wa kwanza hebu ngoja nione itakuaje Leo, ndugu hiyo ni hatari)
17: Uchumba Usiwe wa mda mrefu Sana nayo ni hatari, kama mlifahamiana vizuri kipind I cha urafiki basi uchumba Usiwe wa mda mrefu.
Bwana atusaidie tufanye yote kwa utukufu WA Jina lake!
AMEN!


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post