KAMWE USIOMBE AMA KULAZISHA ABAKI NA WEWE KWENYE MAISHA YAKO, KUMUACHA AENDE KUNA FAIDA HIZI .

Kamwe usiombe ama kulazimisha mtu abaki na wewe kwenye maisha yako kinyume na matakwa yake. Kumuacha aende kunakufungulia milango ya watu bora zaidi kuja kwako.
Maisha ni mafupi mno kuumizwa na kuchukuliwa kama ni option kila siku. Ni muda mzuri sasa wa kujiwekea nafsi yako kama kipaumbele cha kwanza!!
Maana, ipo siku moja mtu atakuja katika maisha yako na kufanya yale yaliyo sahihi ambayo wengine walishindwa kwako. Siku moja atakuja mtu katika maisha yako ambaye hutakuwa na haja ya kumkumbusha kuwa unampemda.
Atakuja mtu ambaye furaha yake ni kukuona ukikuwa kifikra, kiuchumi na kupendeza kimwonekano. Mtu ambaye utamuamini nae kukuamini kwa mambo yote madogo na hata yale makubwa.
Atakuja kuwa rafiki, mfariji, mshikaji, mtu wa karibu na partner wa maisha yako ambaye mtashea nae vitu vidogo mpaka vile vikubwa. Msingi usikate tamaa, kuwa na imani, muombe Mungu.
Usiyumbishwe na maneno ya kukatisha tamaa. Jitamkie yale yaliyo mema!!#reallove #be_sweet #SeeYouAtTheTop 🔥🔥🔥
#How is volume...?


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post