Kama Umeshawahi Kutoa Mimba Fanya Haya Mambo Matatu


Makala iliyopita niliongelea madhara sita ya kutoa mimba, kutokana na jamii yetu kukumbwa sana na janga hili la utoaji wa mimba hasa kwa mabinti wadogo ambao wengi wao wapo vyuoni na mashuleni.

Kutokana na maswali mengi niliyoulizwa nini cha kufanya kwa ambao tayari wameshatoa mimba nimeamua niandike makala hii. Mambo yenyewe ni haya…

Nenda hospitali uonane na daktari; ukitoa mimba kuna madhara mengi yanayofuatia ikiwemo ugumba, na kuharibika viungo vya uzazi.. nenda ukapige picha ya ultrasound kuangalia hali ya viungo vya uzazi, na kama vinaumwa vianze kutibiwa mapema iwezekanavyo kabla mambo hayajaharibika. Pia pima magonjwa mengine ya kuambukizwa ikiwemo ukimwi, kaswende na gono kwani ni magonjwa yanayo ambatana na ngono zembe. usiogope hakuna daktari wa kukupeleka polisi kwa kutoa mimba..

Obama na mtaalamu wa ushauri: kama una mawazo mengi kwanini umetoa mimba na unajutia maamuzi yako au moyoni unahisi umefanya kosa kubwa kwa binadamu au mungu wako nenda unana na mshauri na atakusaidia kurudi katika hali yako ya kawaida.


Chagua njia ya uzazi wa mpango: kuna watu wameshatoa mimba mpaka tano sasa hivi, mimi naona huo ni uzembe kwani kuna njia nyingi sana za kuzuia ujauzito. Kama huwezi kondomu njia ya kijiti ni nzuri kuliko zote kwani siku ukitaka mtoto unakitoa kijiti na kunasa mimba haraka. njia ya kalenda ni nzuri pia ila wengi hawaiwezi na inataka umakini sana hivyo achana nayo..Acha kusikiliza kelele za watu eti njia hizo zina madhara kwani hizo ni imani potofu na ukipuuzia utaendelea kutoa mimba zaidi kitu ambacho ni hatari kiafya. tumia virutubisho vya uzazi; mara nyingi kutoa mimba huharibu mfumo wa homoni za uzazi wa wanawake na  maumbile ya uzazi.hali hii ni hatari na ndio hufanya wanawake wengi kushindwa kubeba mimba siku za usoni. tumia virutubisho vya multmaca ambavyo vimesaidia sana kurudisha hali ya homoni katika kawaida yake na kusaidia kubeba mimba kwa wanaozitafuta.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post