Wakati mmoja nilikua namshauri na kumuelewesha rafiki yangu mmoja ambaye alikua anataka kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu mwezi mmoja tu baada ya kumuambia kuwa anataka kumuoa. Aliniambia kuwa amebadilika, amekua kero, kila siku kuulizia mtakuja lini, kutaka kumpangia mambo na kuwa kero mpaka kuanza kuwaza je huyu atakua mke bora kweli au atakua tatizo?
Labda nianze kwa kusema, jifunze kuacha kulazimishia mambo na kutaka mambo yaende kwa wakati ambao unaoutaka wewe. Kuna mambo mengi ambayo unayakosa na kuuna migogoro mingi ambayo unaiibua kwa kutaka kumlazimisha mwanaume kukufanyia mambo au kufanya mambo kwa ratiba zako. Labda nianze na mfano mmoja ambao huwachanganya wanawake wengi.
Una mpenzi wako ni wa muda mrefu na mara kwa mara umekua ukiongea naye kuhusu suala la ndoa na amekua akikupiga tarehe, ukaamua kuvumilia. Lakini sasa kakuambia kuwa anataka kujitambulisha kwenu au kukuvalisha Pete kabisa. Ile tu kukuambia unaanza kupaniki, unaanza kumpangia ratiba, ameshakuambia mwezi wa Pili nakuja kujitambulisha.
Ameshakuambia nataka nifanye kitu flani kwanza ndiyo nije lakini kila siku wewe unakua mtu wa kuuliza, unakua mtu wa kusema mbona huji, hajakuambia hata uwaambie nyumbani kwenu lakini wewe ushawaambia na unaanza kulalamika kuwa sasa nyumbani watanielewaje wakati nilishawaambia unakuja, unataka kulazimishia mambo, unataka afanye mambo kutokana na ratiba zako na si zake.
Hili ni kosa kwani ukishaanza hivyo unamuambia mwanaume kuwaza mara mbili kuhusu wewe, ni kama unamuambia awaze hivi huyu anafaa kweli kuwa mke au ataniendesha baada ya ndoa. Labda nikuambie kitu, najua una kimuhemuhe, una hamu ya kuolewa na labda tabia zake zinakupa wasiwasi kuwa atakuoa kweli?
Sasa hapa chakufanya si kumuuliza kila siku, hapana unapokua unamuuliza kila siku kitu kile kile inakua kero hasa kama anakupa jibu la kueleweka, punguza wasiwasi na angalia mwenendo wake, angalia kama je kuna kitu chochote anafanya kutimiza ahadi, labda kashaanza maandalizi ya Pete, kutafuta pesa za kuja, kuongea na wazee wake na mambo kama hayo.
Lakini pia wakati unasubiri muda aliousema yeye kufika hembu jipe muda wa kuulizia, kamba labda kila baada ya mwezi mmoja ndiyo nitamuulizia kuwa kafikia wapi? Ndiyo nitamuulizia mipango yake ikoje. Hapa ishu kubwa sio kumuulizia bali ishu ambayo inakera ni kumuulizia kila siku kitu kile kile, unapoulizia kila siku hata kama ni kwa ustaarabu inaonyesha mambo mawili.
Jambo la kwanza nikuwa hujiamini na unaona kama vile kakusaidia kutaka kukuoa na jambo la pili ambayo linakera zaidi nikama unataka kumkalia (kumtawala), kumuamulia na kutokumuacha apumue. Sasa onyesha kujiamini, kwamba pamoja nakua kakuambia atakuoa lakini ndoa sio maisha yako yote hivyo acha kuulizia kila saa au kuanza kunyenyekea nyenyekea kizembe atajua kua unaigiza.
Sasa wakati unasubiri unatakiwa ufanye nini? Hapa ndiyo watu wengi hukosea, kakuambia ana mipango ya kukuoa, kashaleta mahari kwenu na hata kujitambulisha. Kwa wanawake wengi moto huwaka, hapa ndiyo hujiona kama wameshaolewa, kutaka kumthibiti mwanaume na kutaka kuwa wake kabla ya ndoa, wengine hata huhamia kwa hao wanaume kisa barua.
Dada yangu yeye kukuambia nitakuoa, kukuvalisha Pete, kujitambulisha kwenu na kuleta mahari bado hajakuoa. Si mume wako na anaweza kukuacha wakati wowote akaoa mwanamke mwingine, hivyo acha kuwa kama mke. Itakua ngumu sana yeye kukuoa kama utahamia kwake na kuanza kuwa kama mkewe, atakuchoka kabla hata ya kukuoa.
Ukishahamia kwake atakua hana haja tena ya kuoa, lakini ukishahamia kwake kuna vitabia anaweza kuvigundua na kujikuta hatamani kukuoa tena lakini pia ukishahamia kwake utakua ukiishi kwa matumaini tu, kila siku wasiwasi kuwa nitaolewa kweli, hii itakuongezea kulalamika na kuwa kero kwake hivyo akishajitambulisha hembu acha kujipeleka kwake, subiri aje akuoe rasmi na uwe mke wake.
Sasa wakati wa kusubiri hembu endelea na maisha yako, kwamba jiondolee presha ya kuolewa kwa kufanya mambo yako kama kawaida, kama ni kazi fanya, kama ndiyo ulikua unatafuta kazi tafuta na usiache kutafuta kisa umechumbiwa, kama ni biashara basi fanya na kama ni shule nenda. Kumbuka kajitambulisha tu na hajakuoa na wala silazima akuoe.
Sasa hembu jipe muda, usikubali kuishi katika uchumba sugu wa miaka miwili, jipe muda ambao unasema kabisa huyu mtu kashajitambulisha ikipita miezi kadhaa hajatuma watu hata kama siachani na yeye lakini naanza kuondoa wazo la kuolewa na kuendelea na maisha yangu kama bado atakua haeleweki. Usijipe zaidi ya miezi sita au chini ya miezi mitatu.
Kwamba kama uchumba ukipita miezi sita basi unakua ni uchumba sugu, angalau katika miezi hiyo mpange hata tarehe ya harusi. Lakini mpe miezi mitatu ya kujipanga sio kakuambia leo nitakuoa basi kesho unaanza kuuliza mbona hawaji, mbona hiki, mbona kile hapana. Jifunze kuacha kuuliza uliza kila saa, jifunze kuwa na maisha yako ili kujiondolea presha ya kutaka kuolewa.
Post a Comment