KABLA HAMJAAMUA KUOANA MNATAKIWA KULIWEKA SAWA JAMBO HILI KWANZA NDIPO MENGINE YAFUATE.

Kabla ya ndoa mnatakiwa kujadili namna nyote mtakavyoshughulika na familia zenu na mipaka ambayo familia zenu zinatakiwa kuichunga. Uingiliaji wa familia zenu kwenye ndoa yenu ni tatizo kubwa, ndoa nyingi zimeharibiwa na ndugu wa pande mbili. Usione tabu kujadili na mwenza wako kuhusu jambo hili.
Mwanamke anapotumia muda wake mwingi akiwa peke yake nyumbani huku mumewe akimpuuza na kutompa muda wake mwingi, hujikuta kwamba maisha yake yakikosa maana. Hapo anaweza kufikiria kuwa na mwanaume ambaye anaziba pengo hilo na kufanya usaliti.
Unaweza kudhani kuwa unapomsamehe mwenzako unakuwa unamfanyia hisani; ukweli ni kwamba wakati fulani faida ya msamaha haimhusu mwenzako tu, bali inakuhusu wewe. Unaposamehe unaondoa hasira, chuki na mzigo mkubwa kwenye moyo wako. Ukweli msamaha ni dawa ya misuli ya moyo wako.
Wakati wa tatizo wanandoa mahiri hawanyosheani vidole, bali hulinyoshea tatizo husika. Utawaona wakipambana na tatizo badala ya kupambana wao kwa wao. Unaweza kuwa mshindi wa mabishano lakini ukaijeruhi ndoa yako, hapo ni kipi bora?
Nyakati ambazo mara nyingi hutokea ugomvi wa kifamilia ni baada ya kutoka kazini.
Sababu ya hilo ni:
- Kubeba msongo wa kazini kuupeleka nyumbani.
- Mapokezi mabovu ya mwanandoa.
Usitarajie mabadiliko ya haraka katika kuboresha ndoa yako. Inaweza kuchukua muda na kuna mabonde na milima katika kazi hiyo. Jaribu kuangalia zaidi faida ya juhudi yako, na ujikite kwenye juhudi hiyo kwa subira. Ni hatari sana kutarajia mambo yanyooke haraka iwezekanavyo.
Ni bora kupata mabadiliko ya kudumu kuliko mabadiliko ya haraka.
J4real


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post