HUWEZI KUMUONA MKE/MME MWEMA KWA MACHO YA NYAMA...*


jambo la Msingi ni ndoa ni kati ya Mwanamme na mwanamke ambao Moyo wa Mungu umeridhia watu hao waishi pamoja ndoa si kati ya watu walioridhia kuishi pamoja pasipo Mungu kuridhia.....
Ili upate ndoa yenye kibali cha Mungu lazma uwe katika uwepo wa Mungu yaani mahusiano yako na Mungu yawe na mazuri ndipo Mungu atakupa vitu vyema...
Uchumba ni uhusiano salama bila ya ndoa kwanini salama namaanisha uhusiano katika ya mwanaume na mwanamke kabla ya ndoa bila kuvunja sheria ya Mungu kuhusu ndoa yaani kutofanya uhasherati au mambo yanafananayo na uasi ....
UCHUMBA UMEBEBWA NA MAMBO MAWILI IMANI NA NUIO KATIKA YA WATU WAWILI WANAOTAKA KUWA WANANDOA
A....IMANI NI VILE MWANAUME AU MWANAMKE ALIVYO NA AMANI NA UTULIVU NDANI YA MOYO WAKE JUU YA MWENZA NA ROHO AKIMSHUHUDIA NA KUMWAMINISHA KUWA HUYU NDIYE MUNGU AMENIPA... Ndio mana tunasema macho yana mipaka lakini Roho haina mipaka Unaweza ukapenda mwanaume kwakuona mafanikio yake lakini Roho ikakushuhudia huyu mtu si sahihi na Unaweza kumuona msichana ana umbo zuri sana na sura nzuri sana lakini Roho ikakushuhudia huyu si mtu mwema kwangu na sio chaguo langu.... *(MUHIMU HUWEZI KUMUONA MKE AU MME KWA MACHO YA MACHO(TAMAA NA HISIA) BALI KWA ROHO ( IMANI NA MAOMBI MBELE ZA MUNGU*
B.....NUIO NI VILE MWANAUME AU MWANAMKE AMEKUSUDIA NA KUTHIBITISHA ROHONI KUWA UYU NDIE ATAKUWA MME AU MME WANGU... UCHUMBA BORA UZAA NDOA BORA ..ILI NUIO LENU LIWE JEMA NI LAZIMA MNUIE KUWA NA MUNGU PAMOJA KUTEMBEA NA KUFANYA MAAMUZI PAMOJA NA MUNGU WETU NDIPO MUNGU ATATAWALA MAWAZO YENU NA AKILI ZENU NA MTAWEZA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI ( *MUHIMU USIANZISHE NDOA KWA UZOEFU NA AKILI YA BNADAMU BALI KWA MAARIFA ZA KIUNGU NA KUENDELEA,KUMSIkiliza ROHO MTAKATIIFU....*
1 Wakorintho 2:9-10
[9]lakini, kama ilivyoandikwa,
Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia,
(Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,)
Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
[10]Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.
NDOA NJEMA IMEANDALIWA KWA WAMPENDAO MUNGU WALIOJIONA NA KUTAMBUA KUWA SI KWA MASIKIO MACHO YAO AKILI ZAO NA UZOEFU WAO WANAWEZA KUPATA WENZA BALI KWA MUONGOZO WA ROHO MTAKATIFU .RAFIKI MACHO UONA,NJE LAKINI ROHO YA MUNGU UCHUNGUZA NA KUONA UTU WA NDANI WA MTU ..WENGI WAMEDANGANYWA NA MACHO LEO WANALIA WANATAMANI KUVUNJA NDOA LAKINI WANAKUMBUKA NI AGANO LA MILELE ..BASI KATIKA YOTE UFANYAYO BASI NDOA UWE MAKINI SANA KABLA YA KUINGIA MSHIRIKISHE MUNGU NA MHESHIMU SANA MUNGU NA SHERIA ZAKE KUHUSU NDOA
*MUHMU MWADAMU HAWEZI VUNJA SHERIA ZA,MUNGU KUHUSU NDOA LAKINI MWANADAMU UVUNJIKA MWENYEWE NA NDOA YAKE JUU YA SHERIA ZA MUNGU KWA KUTOSHIKA NA KUZIFUATA NA KUTII*
ENDELEA KUMUOMBA MUNGU NA MUNGU ATAKUPA MTU SAHIHI ILA USIJIAMINISHE WA AKILI ZAKO KUWA UPO SAHIHI UTALIA KWA KUSAGA MENO


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post