Hivi unajua Furaha ya mapenzi ni jinsi unavyojiweka na kuishi na mahabuba wako..fanya haya

Furaha ya mapenzi ni jinsi unavyojiweka na kuishi na mahabuba wako ...

Hakuna jambo linaloleta furaha na amani katika
maisha ya kimapenzi kama kumsoma mpenzi wako
na kujua mambo gani ‘humdatisha’ kisha
ukamtimizia.
Hicho ndicho ambacho kimewafanya baadhi ya
watu kufikia hatua ya kusema kwamba, mpenzi
aliyenaye hatamani kumkosa hata kwa siku moja
katika maisha yake.
Wako watu wamekaa katika
ndoa kwa miaka 25 ukiwauliza siku ambazo
wamewahi kutokuwa pamoja hesabu yake kwa
pamoja haitimii miezi 6.
Huo ndiyo ukweli wenyewe. Watu wananenepa,
wanatakata na kutawaliwa na nyuso zenye furaha
wakati wote kwasababu tu wanapatiwa kile kitu
ambacho mioyo yao inapenda.
Wengi ya wapenzi
wa siku za hivi karibuni ukikutana nao wamezeeka,
wamesinyaa, wamepata makunyanzi. Yote hata si
kwamba yanatokana na umri kwenda, lahasa,
wana kidonda moyoni, kidonda kinachowafanya
kukunja uso wakati wote na kupelekea kuzeeka
kabla ya wakati.
Wewe ungependa kuingia katika maisha hayo
hasi? Sidhani, kama sivyo basi leo hii nataka
kukufahamisha mambo ambayo yanaweza
kuyaingiza maisha yako katika hatua nyingine,
hatua ya furaha iliyotimia, furaha itakayopeleka
kutabasamu tena, kuponya donda lako la moyo,
na kuendelea kuonekana kijana japo umri
unakwenda.
Wewe ni binadamu uliyekamilika ambaye hisia
zako zimekutuma kumpenda mtu fulani ambaye
naye ameonesha kukupenda?
Hiyo ni bahati sana
kwako lakini bado unakuwa na jukumu lingine la
kuweza kumfanya huyo uliyempenda akupe nafasi
kubwa katika moyo wake kiasi cha kumfanya
asisikie la kuambiwa juu yako.
Unajua anachokipenda?
Yawezekana mmeishi kwa muda mrefu katika
uhusiano wenu,
je, umeshamsoma mpenzi wako
na kujua mambo ambayo ukimtendea huwa
anachanganyikiwa mnapokuwa faragha au sehemu
nyingine? Kama tayari, nikupe ‘bravo’ lakini kama
bado jaribu kuchunguza, la sivyo utaanza kuzeeka.
Yawezekana kuna siku ulimfanyia mpenzi wako
kitu fulani akakuambia maneno haya, “Napenda
sana unaponifanyia hivi mpenzi wangu, hakika
unanifanya nizidi kukupenda”. Hakuna maneno
matamu kama haya hasa unapoyasikia kutoka kwa
mtu uliyemkabidhi moyo wako, wengine huenda
mbali zaidi na badala ya kusema tu huenda mbele
zaidi na kuonesha shukrani zake kwa vitendo.
Cha kufanya sasa, mfanyie hayo hayo kila mara na
ikibidi wakati mwingine usisite kumuuliza, “Baby
hivi unapenda nikufanyie nini zaidi ili ujue
nakupenda?
Zungumzeni, chunguzaneni kwa yale
yanayowafurahisha, sio afya kuchunguza kama
unaibiwa peke yake.
Kama ni muwazi atakurahisishia kwa kukuambia
yale yanayomdatisha lakini wengine ni wagumu
kusema hivyo itakuwa ni kazi yako kumdadisi,
naamini ukiwa makini utagundua.
Unaziteka hisia zake?
Muwapo faragha, mfanye mpenzi wako azielekeze
hisia zake kwako.
Si wakati wa kuanza
kumzungumzia mtu ambaye unahisi anatoka naye
kwani kwa kufanya hivyo utamfanya aanze
kumfikiria tena huyo unayemhisi badala ya
kukufikiria wewe.
Zungumza naye kwa upendo,
mbusu kwenye shavu, mnong’oneze sikioni,
mguse nywele zake, mtazame kama vile ndio
unamwona leo kwa mara ya kwanza, fanyeni yote
haya bila hata kuvuana nguo.
Chezeni na kucheka
kama watoto, ndio maana mkawa na chumba
chenu wawili tu, hiyo ni faragha yenu, oneshaneni
‘uchizi’ wenu.
Uwapo naye jua kwamba ni wewe pekee mwenye
nafasi katika maisha yake.
Ondoa hisia hasi
kuhusu yeye badala yake muda wote uutumie
kumfanya aamini kwamba unampenda na
umuweke katika mazingira ya kutofikiria kukusaliti
kwa namna yoyote ile.
Wewe ni mtundu na mbunifu?
Utundu wako na ubunifu katika uhusiano wako
unaweza kumfanya mpenzi wako ahisi yupo na
mtu wa kipekee.
Hutakiwi kuwa yule yule kila siku
bali unatakiwa kubadilika na kuwa tayari kujifunza.
Mapenzi yanahitaji shule na shule hii si lazima
uingie darasani. Muulize rafiki yako wa karibu,
mbona nikimfanyia hivi mpenzi wangu anakuwa
hivi? Naamini atakusaidia.
Rafiki huyu awe ni yule
mnayependana na kuaminiana kwa dhati, rafiki wa
kufa na kuzikana, naamini marafiki wa aina hii
bado wapo.
Wasiliana na wataalam wa mambo ya uhusiano au
tembelea mitandao ya mapenzi, huko kuna mambo
mengi yanayohusu namna ya kuboresha uhusiano
wako,
utajifunza na kuwa bora! Kwa taarifa yako ni
kwamba, hata kama una umbo zuri na sura ya
kuvutia, kama si mtundu na mbunifu kwa laazizi
wako huwezi kudumu naye.
Atalazimika kukuacha
na kuangalia mtu mwingine anayejua maisha na
mapenzi.
Jamani mapenzi yana raha yake, kama huamini
waulize akina fulani.

Ukifanikiwa kutengeneza
furaha katika uhusiano wako, hata maisha yako
yatakuwa ya furaha na utashangaa unanenepa tu
hata kama huli chakula.
Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post