*HII NI KWA WANAUME WOTE* ✍✍✍✍✍✍✍


*Wanaume wenzangu, tufanye kazi kwa bidii tutafute hela ili uzee wetu tuwe na uwezo wa kujitegemea. Hakikisha kwenye uzee wako una pesa zako mwenyewe za kukufanya usurvive. Sahau kuhusu watoto, na mama yao kwamba watakutunza. Wewe ndiye stranger pekee kwenye hiyo familia unayoiita ya kwako. Hiyo nyumba ni ya huyo mwanamke na watoto wake. Not yours.!*
*Babu yangu aliniambia kwamba mwanaume aliyeoa ni sawa Tingatinga, ambalo linatengeneza Barabara, lakini ikishakamilika linabebwa juu juu kwenye Lori na kuondolewa, eti likitembea litaharibu barabara. Yani barabara ambayo Tingatinga lenyewe limeitengeneza haliruhusiwi kutembea juu yake.*
*Vivyo hivyo kwa mwanaume aliyeoa. Atajinyima, atajishughulisha, atajizuia kufanya anasa, atakopa, atavaa mitumba ili tu watoto wake waishi vizuri, wale vizuri na kusoma shule nzuri. Siku hizi urithi pekee uliobaki ni elimu bora coz mashamba ziliishaga. Lakini pamoja na yote hayo, bado ukizeeka hao watoto sio wako, ni wa mama yao. Wewe watakuita "Kamzee".*
*Watoto wakiwa na umri wa miaka 10 ndipo mama yao anaanza kuwajaza taarifa zisizovutia kuhusu wewe. Kadri wanavyokuwa ndivyo wanavyoelezwa mambo mengi. Wakifika utu uzima atawaambia "isingekua mimi hamgesoma, yeye alikua ni pombe tu na wanawake" Ukisikia hivyo ujue tingatinga limemaliza kazi yake sasa linakaribia kuondolewa barabarani.*
*Watoto wanapoanza kazi, mzee anakua amestaafu. Wanapokuja kutembelea wazazi, wakiondoka wanampa baba elfu 5 mbele ya mama. Halafu wanaenda jikoni na mama, wanampa hela kwa siri bila mzee kujua. Wakiondoka mama anamfuata mzee na kumwambia sukari imeisha. So ni suala la mzee kuamua kutoa ile elfu 5 aliyoachiwa na watoto ikanunue sukari, otherwise anywe chai isiyo na sukari. Hii ni moja ya sababu inayowafanya wazee kufa mapema baada ya kustaafu na kuacha wake zao Wajane.*
*Nimeshuhudia wazazi wenye watoto ng'ambo wakimchukua mama yao akaenjoy life majuu, na kumuacha baba yao nyumbani akilisha Ng'ombe wao wawili, na kutafuta chakula cha kuku.!*
*Wanaume work hard and save something for yourself at old age. Tafuta pesa kwa bidii, wape watoto elimu bora, wape mahitaji yao muhimu, jenga nyumba nzuri waishi vizuri, lakini ukizeeka dont expect too much from them. Enjoy maisha ya uzee kwa pesa zako mwenyewe ulizochuma ujanani. Kama huna hela utaumwa hata na mbwa wako mwenyewe.!!*
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post