Wasiyoyajua wanaume kuhusu wanawake ni Haya!!!
Raha ya mapenzi!!!!!
Fanya itokee siku moja asubuhi mnapoamka halafu mwambie kuwa alikuwa anakoroma usiku, kisha utashangaa na kugundua baadhi ya mambo mengine kuhusu mwanamke.
Kutoka katika blogi moja ambayo imebobea katika kujadili mambo mbalimbali yanayo zunguka ulimwengu (Dunia) ya Al-amini blogspot, leo nikakutana na baadhi ya mambo ambayo katika ulimwengu huu kumbe wanaume hawayajui kuhusu wanawake, licha ya kuwa wanaume wamezaliwa nao, kukuzwa na wanaishi nao.Tafsiri iliyotumika yaweza kuwa sio rasmi, lakini imelenga zaidi katika kufanya mambo kueleweka. Ombi langu kwako ni kufanya utafiti kisha utakubaliana na mimi au laa!!
1. Wanawake eti siku zote hawana kitu maalum cha kuvaa. Na ndio maana wawezakuta katika kabati la mwanamke limejaa nnguo na mahenbegi kadhaa, lakini asubuhi analalamika hana nguo ya kuvaa.
2. Wanawake ni viumbe wenye kupenda kuona kuwa duniani kuna watu wabaya zaidi yao, na ndio maana vipindi vingi vya kuelezea mikasa ya kinamama walioonewa vinapata umaarufu sana duniani.
3. Wanawake daima si watu wa kukosea. Huamini kuwa, makosa wameumbiwa wanaume tu, na ndio maana wao hata wakikosea, kuomba msamaha ni kwa bahati mbaya japo wakikosewa wasipoombwa msamaha ni tatizo kubwa sana. Hujachunguza?
Sorry baby "wapii"
“ Hapa unajaribu kumuomba msamaha lakini anaonekana kuleta mapozi ya kike, ila anapenda kuombwa msamaha”
4. Wanawake ni wenye kupenda kulia sana tena kila wakati. ILA hawawezi kufanya hivyo kama haupo karibu nao au kama huwezi kusikia kilio chao wanapolia.Chunguza utagundua
5. Wanawake hupendelea sana kufanya manunuzi, maana hili ni moja kati ya mambo ambayo wanaamini wana udhibiti nayo kuliko jambo lolote duniani
jozi ya viatu vya kike
“Utamsikia akikwambia sina viatu kabisa.....wakati vyengine havina pakukaa, ila mwanaume pea nne za viatu zinaweza kumchanganya”
“Utamsikia akikwambia sina viatu kabisa.....wakati vyengine havina pakukaa, ila mwanaume pea nne za viatu zinaweza kumchanganya”
6. Wanawake wengi hupenda kuuliza swali la “Je, naonekana vipi hapo?”, “nimependeza?” japo ukweli ni kwamba hawapendi majibu ya kweli kuhusu swali hili. Mwambie hujapendeza “Utakiona kizaa zaa”
7. Mwanamke anaweza kujipamba akapendeza hata kama anaenda kufanya kazi ya kunyweshea bustani, kusoma kitabu, kwennda jikoni kupika au kutazama tv. Anaweza kukaa mbele ya kioo chake kwa mda ili apate kupendeza. Wanasema mwanamke Urembo
8. Mwanamke anaweza kuendesha gari umbali wa maili hata 100, kwa hofu tu ya kupotea kidogo endapo atatumia njia ya mkato yenye uwezo wa kupunguza safari yake kwa maili 50 nzima
9. Wanawake hupenda sana kuongea kwa simu. Anaweza kumtembelea rafiki yake na kuwa naye kwa wiki kadhaa, na anaporejea kwake muda mfupi baadae akampigia rafiki yuleyule na wakaongea masaa zaidi ya matatu kwenye simu.Chunguza utabaini?
10. Wanawake hupendelea kuchana nywele zao kabla ya kulala. Jiulize kwanini sasa na utaambiwa wewe hujui kitu. Hahahahahaha!!!
Post a Comment