Kama wewe ni mwanamke na unampigia simu mpenzi wako mara tatu kwa siku halafu yeye hapigi hata mara moja kwa siku basi punguza, piga mara moja au hata usipige kabisa, muache yeye ndiyo akupigie mara nyingi, muache yeye ndiyo akumiss zaidi. Jinsi unavyozidi kuonyesha kuwa umechanganyikiwa zaidi kwa mwanaume ndiyo jinsi ambavyo anazidi kukuchoka, simu zako zinatoka kuwa “Baby nimekumiss” mpaka kuwa “Kwanini hupokei simu zangu”
Najua wanawake wengi hudhani kua kwa kumpigia simu mwanaume mara kwa mara, kwa kumtumia meseji nyingi ndiyo kuonyesha kuwa unamjali. Hapana vichwani mwa wanaume ukimtafuta sana ni kama unamuambia kuwa sina kazi nyingine ya kufanya zaidi ya kukupenda wewe na unaacha kuwa mpenzi na kuwa “Yule mwanamke msumbufu” najua wengi mnaogopa na kuwaza kuwa usipomtafuta atatafutwa na wanawake wengine!
Inawezekana kuwa kweli lakini kama mwanaume hawezi kukutafuta hata mara moja kwa siku, hawezi kukumiss hata kwa bahati mbaya inawezekana unahitaji mwingine na huyo anapaswa kubaki kwa hao wengine. Najua huwezi kumuacha lakini hembu acha kujipendekeza wewe, acha kuchanganyikiwa wewe na mpe nafasi ya kutambua thamani yako, mwanaume akishajua huendi popote anaanza kuyaona mapenzi yako kama kero.
Kiasilia wanaume sisi ndiyo tunatongoza na sisi ndiyo tunataka kutaka na si kutakwa, unapomtaka mwanaume zaidi ya anavyokutaka wewe basi jua ni tatizo na hapo ndiyo ambavyo maumivu huanzia hivyo hata kama ni kweli unampenda zaidi lakini hembu vumilia na jifunze kuacha kua wewe ndiyo mtu wa kumtafuta. Acha kuonyesha kwamba maisha yako hayawezi kwenda au huwezi kuwa na furaha bila yeye, kama umemtafuta mara mbili hajakutafuta ya tatu kaa kimya hata kama itachukua mwezi.
Post a Comment