```Familia ni vazi la heshima, vazi lenye kustahili thamani, upendo na kutunzwa, maana wakati wengine wakikuona wanini, mjinga huna kitu, familia inakuona dhababu yenye kustahili kuonwa kila muda.
Familia yako ni vazi ambalo katu haliwezi kukuacha mtupu, hivyo basi kuwa mtu bora zaidi katika familia yako kwa sababu hiko ndio kitu ambacho unatarajiwa kukifanya kwa kiwango kikubwa.
Kwa namna yoyote ile usiruhusu pumbavu za dunia zikakufanya uione familia yako ni kitu chepesi, familia yako yastahili uzito kamili tena uzito wa blanketi kwenye baridi Kali.
Familia yenye upendo na amani ni chemchem ya mafanikio na kujiamini, hivyo kama kuna sehemu mtu anajihisi amani na raha basi ni kwenye familia yake. Ipende, ijali sana na kuithamini famili yako.```🖐🏻
Tuishi humo🙏🙏🙏
Post a Comment