Dada zangu, najua mna hamu sana ya ndoa, najua ukipata mtu ambaye anaongea ndoa! Ndoa! Ndoa! Unachanganyikiwa na kuona mwanaume ndiyo hiyo! Lakini.....

Dada zangu, najua mna hamu sana ya ndoa, najua ukipata mtu ambaye anaongea ndoa! Ndoa! Ndoa! Unachanganyikiwa na kuona mwanaume ndiyo hiyo! Lakini ogopa sana mwanaume ambaye ana haraka sana ya ndoa! Wala sizungumzii ukatili. Lakini kama ukikutana na mwanaume, mmekaa kwenye mahusiano, iwe ni muda mrefu au muda mfupi? Anakazania sana kuhusu ndoa, lakini hamjawahi kukutana kimwili, sio kwamba wewe mwanamke hutaki bali yeye ndiyo hataki, anatoa visababu sababu vingiiii!
Wengi wanajifanya ni watu wa dini sana, anakuambia kuhusu dini lakini si mtu wa kanisani wala msikitini, au dhambi nyingine anafanya sana tyu ila hiyo anaikwepa. Mwingine umemuambia tu sitaki kufanya mapenzi kiutani utani lakini hasisitizi, najua unafurahia kwakua anakuambia kuwa siaki nikuchezee, lakini hali imebadilika, kunaweza kuwa na sababu nyingine zaidi ya hiyo, hembu chunguza kama yaliyomo yamo.
Silazima kukutana naye kimwili lakini ukiwa makini kidogo tu utajua, msisimko wake wakati mko pamoja utajua. Ana kasi sana ya ndoa, anataka kila mtu kujua kama nayeye ana mpenzi, wewe unaona kama ni mapenzi, hapana, chunguza ziadi, wewe ni mtu mzima, unajua namaanisha nini, kuwa makini katika kuchunguza kwako. Nguvu za kiume zimekua ni tatizo kubwa sana na wanaume wengi siku hizi wanaoa si kwakua wanaweza ndoa bali wanataka watu kujua kuwa hawana matatizo, presha za familia zinakua kubwa sana.

NA IDD MAKENGO


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post