Mume wako sio kwamba hataki kufanya mapenzi na wewe bali hawezi kufanya mapenzi na wewe. Mimi ni mwanaume, nakuambia niamini nikisema kuwa hakuna kitu ambacho kinamuumiza mwanaume kama kulala kitandani na mwanamke halafu hhuwezi kumfanya chochote, najau unadhani ni Malaya, labda anafanya kwingine, najua unadhani anakudharau kwakua umezaa, najua unadhani labda anakuona umezeeka, lakini si kweli, w3anaume hatuko hivyo, wanaume kwenye suala la mapenzi hatuna hiyana.
Hivi mtu ambaye anaweza kufanya mapenzi na sabuni na akafika ndiyo achague mwanaume, hapana mume wako hawezi. Sasa unapolalamika kila siku kufanya, unapomsumbua, unaponuna inamzidishia kutokujiamini, inamfanya kuwa na kisirani, ukiendelea hivyo baada ya muda ataanza kuchepuka, kuwa na wanawake wengi, si kwakua huko nnje atakua anafanya hapana, bali ni kwasababu atataka uone kuwa hafanyi kwako ila nnje anaweza.
Hapo utachanganyikiwa zaidi kwani kumuacha hutaweza, atakunyanyasa na wkaati mwingine vipigo juu, kwasasa wakako hajafikia stage hiyo. Kwa maana hiyo, fanya hiyo mara moja kwa mwezi, ifanye vizuri na ridhika, hili ni suala la kiakili tu, ukiitengeneza akili yako kuridhika mara moja basi hutaona shida, usipoitengeneza hivyo kila siku utakua unalalamika na hutapata. Ndoa ina miaka 10, mna watoto wawili, shukuru Mungu imetokea wakati mna watoto kwani ingekua kabla basi ungekua na kisirani mara 100 zaidi.
MTEJA; Lakini Kaka mimi nikae mwezi nafanya mapenzi mara moja hapana, nataka niondoke.
IDDI MAKENGO; Anakupiga?
MTEJA; Hapana.
IDDI MAKENGO; Anakunyanyasa?
MTEJA; Hapana.
IDDI MAKENGO; Anahudumia familia?
MTEJA; Hapana, lakini Kaka mimi sikufuata hivyo, hata kwetu chakula kipo nilifuata tendo la ndoa.
IDDI MAKENGO; Anakupiga?
MTEJA; Hapana.
IDDI MAKENGO; Anakunyanyasa?
MTEJA; Hapana.
IDDI MAKENGO; Anahudumia familia?
MTEJA; Hapana, lakini Kaka mimi sikufuata hivyo, hata kwetu chakula kipo nilifuata tendo la ndoa.
IDDI MAKENGO; Najua ila shida ni moja, nimeongea na wewe, tofauti na hasira na kisirani ukweli nikuwa huwezi kumuacha huyo mwanaume, narudia, huwezi kumuacha, kuna mwanamke kukiongea naye inabidi ubembeleze kabisa kuwa abaki kwakua ndoa yake ni nzuri, ila wewe nina uhakika asilimia 100 humuachi huyo mwanaume.
MTEJA; Kwanini unasema hivyo Kaka? Mbona nina kazi yangu na naweza kujitegemea?
IDDI MAKENGO; Shida sio kazi Dada, shida nikuwa huyo mwanaume wako kakudekeza sana na wewe unamtegemea sana, kiuhalisia una kazi lakini hujui kujitegemea na unalalamika si kwakua umemchoka mume wako bali ni kwakua huna kitu cha kulalamikia. Mume wako hajaishiwa nguvu kabisa, fanya hiyo mara moja au mbili.
MTEJA; Kwanini unasema hivyo Kaka? Mbona nina kazi yangu na naweza kujitegemea?
IDDI MAKENGO; Shida sio kazi Dada, shida nikuwa huyo mwanaume wako kakudekeza sana na wewe unamtegemea sana, kiuhalisia una kazi lakini hujui kujitegemea na unalalamika si kwakua umemchoka mume wako bali ni kwakua huna kitu cha kulalamikia. Mume wako hajaishiwa nguvu kabisa, fanya hiyo mara moja au mbili.
Muhimu usibadilike sana, wakati mwingine mdai tendo kuwa unataka na akisema amechoka nuna kidogo ili asione kuwa umebadilika kisha endelea na msiah, amua kuiofurahia hiyo mara moja basi. Mimi si mgumu kukuambia ondoka, hiyo ndoa ingekua imekufa ningekuambia imekufa, kingine katika kitabu changu cha ‘Mwanaume’ nimeelekeza vyakula, mpikie mume wako, nimeelekeza namna ya kufanya mapenzi ilia kufikishe kileleni hifunze, acha kisirani na maisha yataendelea.
Ila sasa siwezi kukulazimishia, ingawa najua hutaondoka ila ni hivi, hembu jaribu ushauri wangu kwa miezi sita, kama hautafanya kazi nipigie simu niambie nimechoka nitakushauri namna ya kuondoka.
MREJESHO; Uliniambia nikutafute baada ya miezi sita, nimechelewa ni karibu mwaka sasa, nikisoma visa vya wengine nashukuru Mungu niliamua kufuata ushauri wako, mimi na mume wangu tuna amani na nadhani kelele zangu zilikua zinamuondolea kutokujiamini ssa hivi hata mara mbili tunafanya na hatuna migogoro na sasa hivi nnina ujauzito mwingine.
KUTOKA KWANGU; Dada zangu, si kila siku utapata kila unachokitaka, wakati mwingine utapoteza, pima unachokipata na kile unachokitaka kisha acha maisha yaendelee. Kuna vitu vya kuvumilia na kuna vitu vya kukimbia.
Nina vitavu vitatu, cha Biashara 50, Ndoa Yanugu Furaha Yangu na Mwanaume. Kitabu kimoja bei yake ni shilingi elfu kumi, unalipia kwa M-Pesa No. 0742-381-155 au Tigo Pesa No. 0657-552-222 jina ni Iddi Makengo hakuna jina jingine. Ukishalipia utatumiwa kwa Whatsapp, Email au Facebook, hakuna vitavu vya karatasi ni digital tu.
Post a Comment