DADA YANGU NAOMBA UZINGATIE HAYA YA MSINGI.

Mume wako amefariki, Pole, kwa bahati amekuachia mali kidogo, labda ni duka, labda ni nyumba, kampuni na Biashara nyingine yoyote ile, amekuachia kitu cha kukuingizia kipato. Una watoto, najua una mahitaji ya kimwili pia, umpweke, najua unaumia, najua unatamani mtu wa kukufariji, mume kafa, hutaishi milele, lakini kuwa makini, narudia kuwa makini.
Utakutana na mwanaume ambaye anafanya kazi lakini kipato chake ni cha kawaida, atakuonyesha upendo ambao hujawahi kuonyeshwa, yaani mpaka utajihisi kuwa uko mbinguni. Mwingine ana pesa, tena ni mfanya Biashara mkubwa kuliko wewe, ana uzoefu,a anijua hiyo Biashara, inawezekana hata alikua ni rafikiwa mume wako, au mtu mwingine tu, lakini anakusaidia, anakupa mawazo ya akili sana, namna ya kuapata wateja, namna ya kuendesha Biashara na mambo kibao.
DADA YANGU; Kaka umjane unapaswa kuzingaria mambo ya fuatayo, najua uimechanganyikiwa unamuona huyo mwanaume kama malaika ila zingatia haya mambo;
(1) Mwanaume akikupenda akitaka kukuoa basi akupeleke kwake, kamwe usiruhusu mwanaume mwingine kuingia kwenye nyumba ya marehemu mume wako kwani mwanaume amabye anakubali kufanya hivi kuna uwezekanao mkubwa sana ikala kwako, akikupenda akuoe wewe na si kukuoa wewe na mali zako!
(2) Biashara zako ni kwaajili yako na watoto, yeye si Baba yao, hana uchungu naoa, narudia hana uchungu nao, hata kama ana uzoefu wa Biashara basi aishie kushauri tu lakiniaissimamie, yaani hata dukani asiingie na matumizi ya pesa ufanye wewe, narudia matumizi ya fedha ufanye wewe.
(3) Kua makini na hati za nyumba yako, narudia kua makini, usichukulie mkopo, hata kama akija na kukupa wazo zuri la Biashara namna gani, kamwe usichukulie mkipo na kumpa pesa, huyo mtu akitaka afungue baishara zake,a tafute chake kama wanaume wengine na si kutumia za mume wako.
(4) Kama angejua Biashara asingehangaika na vimali vya mume wako, narudia, inawezekana ana Biashara, tena kubwa kuliko yako, unamuona kama kafanikiwa, huyu unamuamini na unaona kabisa kuwa hawezi nidhulkumu. Niamini nikikuambia kuwa mwanaume mwenye pesa hahangaiki na vibiahsara vya marehemu, ana pesa ndiyo ila hazitoshi, usipokua makini utauza mpaka nyumba na utaishia kulia tu!
(5) Kama ana mke huyu ndiyo shetani kabisa, aisee hamuachi mke wake, anaweza kumtelekeza kwa muda tena na wewe ukamtukana, ukaona kama wewe nio raha, labda wewe una cha maana zaidi kuliko mke wake basi akasimamia mali zazko, ila niamini nikikuambia kuwa akishakupukunyua pesa zote atarudi kwa mke wake, tena wengine wanaongea na wake zao kabisa kuwa huyu mjinga tumchune, najua huamini mpaka yakukute.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post