"AKIKUTAFUTA KWA KUJISIKIA NA WEWE MTAFUTE KWA KUJIFIKIRIA MUENDE SAWA"

Mawasiliano ni zaidi ya mazungumzo, nawasiliano ni zaidi ya kupiga simu na kujuliana hali. Mawasiliano yasiyojumuisha hisia tamu, lugha tamu, pumzi tamu, sifa tamu na ulimi mtamu basi hayo si mawasiliano.
Mawasiliano yanayojikita tu kwenye ulalamishi mwingi hayo si mawasiliano. Ndio maana niliwahi kusema unaweza kuwa mume au mke, lakini usiwe mwanandoa.
Kwenye siasa kuna mbunge (member of parliament) na mwana-bunge (parliamentarian). Hata kwenye ndoa kuna mume au mke na mwanandoa.
Mwanandoa hufanya mawasiliano yenye sifa nilizozieleza hapo juu, lakini mume au mke huzungumza na kufanya mawasiliano butu. Mwanandoa huijua ndoa kindakindaki tofauti na mke au mume.
Je wewe uko upande gani?
"AKIKUTAFUTA KWA KUJISIKIA NA WEWE MTAFUTE KWA KUJIFIKIRIA MUENDE SAWA"
Ni vigumu kuona mema kwa watu wasio wema. Ukitaka kuona mema, kaa na watu wema, na useme yaliyo mema, ndipo yaonekane mema. ata wasipoona ni mema endelea kutenda mema.
Kuna wakati hupaswi kulia mbele za mtu aliye kuumiza,
Unapaswa kulia mbele za Mungu anaejua ni kiasi gani umeumia, na kuimba nyimbo za sifa na shukrani kwa kukupitisha katika hayo yote.
Moyo wako usiugue juu ya mwanadamu ...moyo wako uugue juu ya kumtafuta Mungu ataka kama mwanadamu kakusaliti,kakupotezea muda, kakuumiza kiasi gani achana nae komaa na Mungu ndie kila kitu
"Usimfitinishe mtu mwingine ili tu wewe upate nafasi kwa fulani" wewe fanya tu vizuri utapata nafasi na kibali.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post