Acha Kusukumwa na pesa katika Kila Kitu unachofanya

❤️️❤️️❤️️: JINSI YA KUMJUA MPENZI LAGHAI NA MUONGO

Mafanikio ni kitu cha ajabu sana, wakati watu wengi wa kiangalia pesa kama mafanikio wapo watu ambao huangalia kuwa na furaha katika mapenzi kama mafanikio, mimi naangalia kufanya kitu ninachokipenda kama mafanikio. Napenda kuandika na naweza kukaa kutwa nzima bila hata kukumbuka chakula nikiandika tu.

 

Kwangu kuandika kitu na watu wakakisoma ni mafanikio bila kujali napata pesa au la. Katika maisha ukianza kupima mafanikio yako kwa kuangalia kiwnago cha pesa unayoingiza basi jua unaelekea kubaya, iwe ni kazini, katika biashara au katika mapenzi.

 

Hii ni kwasababu kuwa kama unasukumwa na pesa basi unaweza kufanya kitu chochote kile ili tu kupata pesa ya zaida lakini kama unasukumwa na upendo wa kile unachokifanya basi nirahisi kufika mbali kwani utakifanya vizuri na siku zote pesa hufuata vitu vizuri.

 

Labda nitoe mifano mitatu katika mambo matatu, kwaza ni katika kazi, pili ni katika biashara na tatu ni katika mapenzi. Katika kazi kwa maana ya ajira, kama akili yako ikiwaza pesa tu, yaani nunafika ofisini badala ya kuwaza majukumu yako unawaza pesa tu nirahisi kwanza kuharibu kazi za watu, pili kuingia tamaa za rushwa na tatu kuipoteza kazi yenyewe.

 

Ukisha pata pesa utawaza kuzitumia na si kutimiza majukumu ambayo ndiyo yalikusababishia kuzipata hizo pesa, hii ni mbaya kiajira. Lakini katika biashara ni rahisi kumuuzia mteja kitu kibovu kwakua tu unataka pesa na ukishafanya hivyo mteja akifika na kukutana na kile kitu kibovu basi inakuwa ndiyo mwisho wake kurudi kwako na unaweza kuwa ndiyo mwisho wa biashara yako.

 

Tukirudi katika mapenzi, kama akili yako iko kwenye pesa tu basi unaweza kujikuta unakuw atayari kufanya mapenzi na mtu yeyote yule kwakuw atu anapesa. Unaweza kufanikiw akuzipata lakini kwa gharama gani? Ubatya wa pesa za namna hii inakufanya kuw amtumwa wa ngono, kwamba ili ueendelee kupata pesa inabidi ufanye mapenzi na wanaume wengi au wanawake wngi ambao hawakuvutii ili kutimiza mahitaji yako.

 

Unaweza kuona ni kitu cha furaha kwa wakati huo lakini kadri umri utakavyokuwa unaenda na kujikuta hujafaidika chochote zaidi ya kujidhalilisha ndipo utaanza kujuta. Fanya kitu kwakua unapenda kukifanya na fedha zitakufuata baadaye ukiwa unafanya kitu ambacho unakipenda. kwa kawaida pesa haileti furaha bali huahirisha huzuni.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post