```Ifike wakati uhisi kabisa yaani uwe na uhakika kwamba upo kwenye mahusiano yanayoeleweka, mahusiano yenye tina na muelekeo chanya. Sio kila anaekutongoza anakuoenda kwa kumaamisha au ana nia ya dhati ya kuwa na wewe, wemgine hawapo serious na wala hawajui nini maana ya upendo.
Wengi hawayathamini mahusiano na ndio maana huwaumiza wenza wao na kuwaachia vidonda moyoni bila kujali muda waliowapotezea, hisia zao na hata maumivu watakayoyapata kwa kuchezea mioyo yao.
Cha kufanya wewe kabla hujaingia kwenye mahusiano jitahidi kujua tabia na mapungufu ya huyo mwenza wako na kama unaona utaweza kuishi nae jinsi alivyo basi sawa ila kama utaona mtashindwana kutokana na tabia yake basi chunga huruma yako isije kukuponza.
```🖐🏻
```🖐🏻
Post a Comment