Mapenzi yana kawaida hii. Endapo hujaanza kuishi na mtu yaani hujaingia naye katika mahusiano huwezi kuona ubaya wake na pia kila zuri litakuwa kwake. Lakini kipindi ambacho unakuwa naye karibu shetani hujisogeza karibu na wewe utaanza kuona kila baya duniani, analo mpenzi wako. Cha msingi ni kuomba Mungu na kufanya jitihada za dhati ili uhusiano wenu uzidi kudumu katika furaha, amani, upendo, uaminifu na mafanikio.
Kuvumiliana na kurekebishana (kuelimishana) ni nguzo kuu 2 katika kudumisha ndoa au uhusiano, hii ni kutokana na ukweli kuwa mmekutana mkiwa watu wazima kila mtu na meno yake 32 , kila mmoja amekulia katika mazingira na malezi yake hivyo tabia nyingine za mwenzio hutoeza kuzijua kirahisi hadi utapoingia rasmi katika ndoa au kuanza maisha nae. Huenda ukashtushwa mno na tabia zake zitazojitokeza ila tambua binadamu ndivyo tulivyo kubali kuendana nae muelimishe mshauri umrekebishe maana tayari ndio wako huyo maji ushayavulia nguo shariti uyaoge, mvumilie wahenga husema UKIONA NDOA IMEDUMU UJUE MMOJA KAJIFANYA BWEGE.
Hata ukisema uachane nae utafute mwingine utakuta nae ana mapungufu yake vile vile maana hakuna binadamu aliyekamilika, cha msingi ni kuvumiliana na kurekebishana, haina haja kugombana kila siku kaeni chini muongee muyamalize kosoaneni na kushauriana ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima kati yenu.
Pasipo kuvumiliana na kurekebishana mtaishia kulumbana kila kukicha mtanuniana na hata kupigana, mtabaki mkilalamika na kusema NDOA NDOANO, NDOA STRESS TUPU n.k ila ukweli ni kwamba ndoa ni tamu mno iwapo mkivumiliana mkirekebishana kila mmoja akabeba madhaifu ya mwenzie mkaishi kwa upendo kama mwili mmoja hakika furaha na amani vitatawala maisha na familia yenu daima mtakua na ndoa mubashara yenye mafanikio.
Nakutakia siku Njema, Mungu Akubariki na kukulinda
Post a Comment