WAMEHARIBU NDOTO ZANGU NA MWANANGU


Image result for mapenzi wakubwa
Asubuhi niliamka na kumuogesha mwanangu wa pekee ambaye kwangu ndiye mboni yangu, kila nimtazamapo najiona mimi, alikuwa hana mama kwani mke wangu alikufa akiwa anajifungua.
"Soma mwanangu wewe ndiye mwanga wangu ". Licha ya kuwa alikuwa bado anasoma kindergarten ila nilikuwa nategemea mengi kupitia yeye. Kila nikimwangalia nilikuwa kama namwona marehemu mke wangu.
Baada ya kumuogesha nilimpa uji wake wa lishe na kumnawisha kisha nikamvalisha sare za shule na kumpandisha kwenye pikipiki yangu hadi shuleni kwao. Nilitamani nimsubiri hadi muda wa kurudi ukifika lakini nilipaswa kufanya kazi pia.
"Dad I love you" mwanangu alisema nilimbeba na kumbusu kwenye paji lake la uso na kumuachia kisha nikaondoka kwenda mishe mishe za kila siku. Yaani nilikuwa nafanya kazi ya bodaboda.
Licha ya kazi yangu kuwa ni kuendesha pikipiki ila nilijitahidi kumpeleka mwanangu kwenye shule nzuri ili maisha yake yaje angalau kuwa mazuri, sikutaka aje achezewe na wanaume hovyo.
"Nitajitahidi mwanangu aishi maisha ya ndoto zangu, nitatumia gharama yeyote niwezayo ili mwanangu afurahi ". Kwakuwa mwanangu alikuwa anapata chakula shuleni kwao, hivyo mchana nilikuwa sirudi nyumbani.
Siku hiyo baada kuzunguka mjini, kama kawaida yangu niliendesha pikipiki hadi shuleni kumchukua mwanangu, ila niliambiwa amerudi. Nilichanganyikiwa kwani mtoto asingeweza kufika nyumbani pekee yake.
Nilianza kumtafuta mtoto huku nikiwa na wasiwasi mkubwa, nilianza kuhangaika kwani mtoto wa miaka mitatu kufika nyumbani ilikuwa kazi isitoshe hata shule alianza baada ya kuona hana mtu wa kukaa naye nyumbani.
Kwasababu ya hofu yangu nilitoa taarifa polisi juu ya kupotelewa na mtoto, licha ya kuahangaika sana mtoto hakuonekana, nilianza kulia bila mtoto maisha yangu yasingeenda hata kidogo kila kitu kingeharibika kwangu.
Baada ya kuhangaika sana mtoto alikutwa amelala kwenye mahindi ambayo yalikuwa yamepandwa karibu na nyumba za watu, ila mbali toka shuleni na mtoto alikuwa ameumia sana sehemu za siri na damu ilikuwa imevilia.
Alipelekwa hospitali ambapo walimsafisha na kumshona nyuzi kadhaa na ilionekana kuwa amebakwa tena na mtu mzima, niliumia sana kuona yote hayo yanatokea kwa mwanangu kipenzi.
"Baba walikuwa na gari yao, wakaniambia wananipeleka nyumbani ila wakanipeleka kwao na kunilaza kitandani na wakaanza kuniingiza huku ". Nillila sana nilitamani nijue ni nani ila haikuwezekana.
Baada ya kupata nafuu aliruhusiwa, ila nilikuwa sina amani, baada ya miezi mitatu nilienda na mwanangu hospitali na kupima na ikagundulika mwanangu ameathirika na virusi vya ukimwi, nililia sana.
Mwanangu ana miaka tisa sasa kila nikimwangalia nabaki nalia kwani watu wabaya wameharibika ndoto zangu na mwanangu, inauma sana nitamwambia nini mwanangu.
Kuna nafikiria niache kumchukilia dawa ili afe akiwa bado mdogo, lakini kwa jinsi ninavyompenda siwezi fanya lolote I LOVE YOU MY DAUGHTER BINADAMU HAWAFAI NAWACHUKIA.
AsUBUh NJEMA WAPENDWA


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post