Basi usivione ukatamani kuvipata, Ni bora kuvikosa vilivyo Bora lakini ukawa na utulivu wa NAFSI! Kuliko kupenda ambavyo tayari wenzio waliishagharamia VINA GHARAMA HIVYO💏
Kuunda mwenyewe na kujenga kama upendavyo awe ina Maana sana, Kwani aliyejengwa na kupangika huyo ATAKUGHARIMU hatakuwa kwenye mwendelezo wa penzi lako bali atakuwa nawe kwa sababu zake, Hujui alikotokea mpaka kuwa hapo JE ALIYEMFANYA AWE HIVYO ATAKUWA TAYARI KUKUONA UKITAKA KUMPOKONYA ZAO LAKE?
Fahari ya MOYO ni yatokanayo na haja zake, lakini kataa kuwa na haja na vya wengine, Haina maana ya kutaja MIGOGORO yao lakini wawili wakiishakuwa MWILI MMOJA Kuna ambayo yanawafanya kuvumiliana, Muungano unaojengwa na MAPENZI huwa na NGUVU itokanayo na uhitaji wa NAFSI.
Ishinde TAMAA kwa woga wa kuingilia PENZI LA WALIOPENDANA KABLA YAKO utakuwa umejiepusha na STRESS za maswali ya Kwanini, Kwani tayari NIA pamoja na THUBUTU Uko navyo Basi JITWALIE WA KWAKO na umtengeneze kulingana na MUONEKANO ambao unauhitaji, Ni rahisi kumtengeneza awe kama upendavyo ili tamaa ya kuangalia walio na ubora uutakao ikuishe, Kubwa katika kumpendezesha ni KUMPA AMANI ili nafsi yake itulie niamini HAKUNA MTU MBAYA DUNIANI labda kwa ulimwengu ujao, Kuliko kupenda muonekano wa Mtu huku ukijua wazi SIO KWA UPENDO ila kwa tamaa wakati wapo wazuri waliojitengeneza wao ili uje kulipia HAO WANAKUFAA ila usijaribu kucheza na HISIA za Mtu ambaye ana UPENDO nawe ni hatari🚫
Tamaa ina gharama zake na mara nyingi TAMAA YA MAPENZI hiyo ndiyo ambayo IMEWAGHARIMU WENGI na kuwaacha njia panda wala wasijue UKOMBOZI WAO utapatikana lini.
Uzuri pamoja na Ubora wa Mtu unatokana na MATAMANIO YAKO Basi ujue yeyote ni MZURI kwa namna unavyoweza kutaka awe Basi MFANYE AWE😎
#Elista_Kasema_ila_Sio_She
Post a Comment