UZURI WAKO UNAMKABIDHI NANI??

Uzuri wako unamkabidhi nan? Unajua kwamba ukikosea kua na mtu sahihi kwenye mahusiano unaweza ukashindwa hata kuona thamani ya uzuri wako?
Tukiachana na uzuri wa nje tambua kwamba una uzuri wa ndani ambao utakufanya uthaminike na pia kuheshimiwa na yeyote. Mwanamke unatakiwa kuwa kama sumaku! Sumaku inavuta vitu vya chuma tuu hivyo nawe yakubidi umvutiee mwanaume mwenye sifa na vigezo vya kujali utu na sio vitu.
Mwanaume mwenye hofu ya Mungu, busara, anayetenda matendo mema na mwenye upendo, kukali na moyo safi.
Mwanamke ukitaka uzuri wako ununuliwe na vitu, mwonekano pamoja na umaarufu usije kulalamika utakapoumizwa na kupotezewa muda. Kumuomba Mungu akupe mwanaume sahihi ni jambo jema sana ila usiishie tuu hapo bali tumia na akili aliyokupa Mungu kumjua huyo aliye sahihi kwako. Fedha na mali za wanaume kisiwe kigezo cha kumpa usahihi mwanaume.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post