Utajuaje Kama Kaumbwa Kwa ajiri Yako, Ndie Anaefaa Na Mwenye Sifa Za Kuwa Mke Ili Kuvalishwa Ile Pete?


Utajuaje Kama Kaumbwa Kwa ajiri Yako, Ndie Anaefaa Na Mwenye Sifa Za Kuwa Mke Ili Kuvalishwa Ile Pete?Baada ya miezi kadhaa kupita toka mwanzo wa mahusiano, swali linalofatia kichwani je huyu ni mke au ni bomu jingine unalotakiwa kuepukwa? wanaume wengi wanapata mawazo sana kutaka kujua je msichana alie nae ndo hasa anapaswa kuitwa mke na kuapa kwa mema na mabaya au ni mpitaji tu, na iwapo akipewa cheo hicho sio siku nyingi ndoa itavunjwa na kutosana?, hii inawafanya wanaume wengi kutumia mda mrefu sana kufikiria mambo mpaka wakatangaza ndoa.  

               Kiumeni.com imekuandalia njia nzuri ya kumsoma na kupata majibu ya maswali yako ni kufuata sifa zilizotolewa na wanandoa baada ya utafiti wa muda mrefu...

  • Unamwamini....
Kuna usemi ambao kila mwanaume ameshapata kuusikia, ''mwanamke si mtu wa kumwamini!'', kama amakufanya usiendane na huu usemi basi jua ulipo ndo sehemu hasa unapotakiwa kuendelea kuwepo, mke ni yule anaekupa sababu zote za kukufanya umuamini, mtu ambae utamuachia dhamana ya kila kitu chako na kukufanya moyoni ujiamini, na yeye anakuamini kwa kila ishara anayokuonyesha.
  • Anaendana na rafiki zako....
Ukarimu sikuzote haujifichi, na kiongozi bora ni yule anaekubalika, ukiwa na msichana mzuri wa tabia sikuzote wa kwanza kukuambia ni rafiki zako maana ndio wanao kujua  na kukufahamukizuri hakifichiki na wewe lazima utaona uchangamfu wake hata ukipata ugeni nyumbani, tabasamu na vicheko na furaha vinakuwemo ndani ya nyumba.
  • Ananjia zake binafsi zinazoendana na familia yako yenye mapungufu...
 Siku zote mama na baba yako ndo waliokukuza na kukufanya uwe kama ulivyo, na kama yeye na mama yako nyumbani wanaendana kicheko na furaha haziishi, kaka hapo sidhani kaa unalakuongeza, watu wazuri wa kuwasoma watu ni wazazi wako na siku zote wazazi wako hawawezi kukuficha maana wanataka maendeleo yako.
  • Unasahau marafiki zako...
Maisha yako yote imekua wewe na marafiki, zile mitoko uliyokua unafanya, story za hapa na pale na marafiki  ukiona zimeisha, mawazo tena na wao hamna zimebaki hi tu wakati unawahi mihadi ya kumuona mamii ujue kaka hapo umekolea na mapenzi na unaenedelea vizuri na juhudi zako za maisha ya furaha, na ndani ya moyo ukiwa na furaha na kuona anakujari na kukupenda basi huyu ndie.
  • Anakuheshimu na unamuheshimu...
Heshima ni msingi wa mapenzi, nyumba na familia, hamna kitu cha msingi kama kuheshimiana na kila mtu kujua mipaka yake na kama na hilo pia analitimiza kaka kilichobakia ni kutafuta pete na kukamilisha mambo yanayofuatia!.
  • Mnaendana na anakukamilisha wewe...
Familia nyingi zimekua zikivunjika kwa tofauti ndogo ndogo za mawazo na maneno, unakuta bwana anataka hivi uku mke nae anamsimamo wake, ni vizuri kusomana ili mpate kuendana vizuri, na ikiwa ukampata mwenza ambae mnaendana kimawazo na fikra ni ukamilifu tosha unao uhitaji, maana mawazo yakisha enda ni kumuomba mungu awaongezee maisha marefu maana hamuwezi kupingana na kubomoa, bali ujenzi wa maisha mazuri ndo utakaofatia.
  • Unamsahau mpenzi wako wa zamani...
Sidhani kwa yote hapo juu kama unaweza hata kumkumbuka mpenzio wa zamani, nadhani utakachokua unawaza ni alikua wapi huyu malaika toka awali, wapumbavu wakawa wananiumiza moyo na kuuchefua moyo wangu.
                Ndoa ni kitu kikubwa na kizito kinaitaji muda kumuangalia mpenzi wako ili usije kosea ukaoa baada ya siku kadhaa ukaanza kujuta, Anko wangu hua ananiambia ''HELI UKOSEE KUJENGA KULIKO KUKOSEA KUOA, MAANA UKIKOSEA KUJENGA UTABOMOA SEHEMU ULIOKOSEA NA KUREKEBISHA UPYA!, ILA UKISHAOA HAMNA MAREKEBISHO''.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post