Macho ni madanganyifu sana na muda mwingine huuyumbisha moyo, Moyo nao Kuna wakati hukosa ustahamilivu Kwani hisia huleta shida mwilini, Una mke ama mume na pengine ndoa ama mahusiano yanakutesa na kukukosesha furaha mpaka unakata tamaa kuendelea! Unakutana na mtu na macho yako yakakusababisha upate mfadhaiko na hisia kukosa ustahamilivu mwisho wake ni KUSALITI. Muonekano wa mtu sio uhalisia wa kile kinataka kukuingiza katika usaliti, Wapo watu wamejaaliwa vyote Yaani muonekano lakini pia wakaleta burudani kwa wenzi wao, Kumbuka bado Uko kwenye Mahusiano ama ndoa pamoja na changamoto unapitia... Mpira siku zote dakika 90 haijarishi umefanya mazoezi mwezi mzima neno moja USHINDI na hapo ndipo huwa pagumu, Unajiandaa kisaikolojia kuwa leo nakutana na MPENZI MPYA saa zingine hata nguo za ndani mpya, Umenyoa nywele kila mahala, Perfume kali umejipulizia mwenyewe unanukiaaaa! Faraghani mpo wawili, Nguo zote kabatini kama hamjaning'iniza nyuma ya Mlango, Bwana wangu weeeee YAANI HAKUNA JIPYA unajuta kujiandaa kote kule bora hata usingesaliti maana huyu ndo bomu kabisaa afadhali na wakwangu, Hapo ndo huwa patamu sasa, Zoezi la dakika 10 kama sio robo saa linakuingiza katika usaliti na mbaya zaidi UMECHAFULIWA TU na kuachiwa shombo... Mapenzi ni kuelekezana na kuwekana wazi juu ya kile unaamini ndicho huleta BURUDANI kusaliti sio tiba katika mapenzi Kwani waweza kuwa husemagi vile unataka ufanyiwe, Sio wote ni watundu kujuwa wapi aguse iwe burudani kwako, Sema unapenda mkao gani kitandani, Mwambie vile unataka afanye kuliko kuugulia ndani na kutafuta michepuko, Jichunge na kuusema ule msemo wa Waswahili usemao USIACHE MBACHAO........... 😅😅😅😅😅😅
Michezo, Matokeo, ajira, Livescore,msimamo wa ligi
Post a Comment