USIYALEWESHE MAHUSIANO YAKO kama mlevi wa pombe alewapo kupoza stress😎

Image may contain: 2 people, people sitting, outdoor and nature
Kama ilivyo NGUMU KUTATUA MATATIZO KWA KUNYWA POMBE ndivyo ilivyo ngumu mno kwa;
Mtu kutafuta mbadala wa Mtu kwenye MAPENZI ili kupunguza ama kufubaisha matatizo ambayo yapo kwenye UHUSIANO WAKE
Ni kweli kabisa Kuna stress kwenye MAHUSIANO na Kuna muda mtu unaweza kujikuta unakata tamaa ya kuendelea BETTER ku-stop🚫 kuliko kuendelea huku ukijua kabisa UHUSIANO WAKO USHAINGIWA SHUBIRI😭
Kinachotufanya kuyalilia MAHUSIANO ni ule urafiki ambao upo kwenye MAPENZI na huo ndo husababisha AMANI pamoja na FURAHA lakini kama unaona mienendo ya UHUSIANO/NDOA yako hauleti ile maana halisi ya mtazamo wako KUMBE UNA CHEAT ILI KUFAIDI NINI👂
Huwezi ku cheat ili umbadiri Mtu kwamba aendane na ulivyokuwa unatarajia zaidi unajiongezea MATATIZO TU.
Huo ndo ulevi mbaya kuliko hata ulevi wa pombe🍻 Maana mlevi wa pombe akinywa pombe husahau matatizo yake na pombe ukiisha matatizo yapo pale pale ila ujue USIKU ALILALA😅
Lakini ulevi wa MAHUSIANO huo hauna mbadala zaidi ya MARIDHIANO AU KUACHANA kwa sababu tabia ya Mtu ni kama ngozi, Kwamba Mtu anaweza kusema HATORUDIA ikawa kweli kama alikosea kwa bahati mbaya, ila kama Makosa yake hujirudia na neno SAMAHANI likawa kama nguzo ya wewe kumsamehe MY FRIEND kuiona nafuu ya UHUSIANO wako kwa Mtu wa aina hiyo ni sawa na kungojea MIMBA KWA MGUMBA
Ndo maana nikasema;
"USIYALEWESHE MAHUSIANO YAKO"
Kama umejaribu kuweka Sawa penzi lenu na huoni mabadiliko zaidi unaumia kila siku njia sio wewe kutafuta mbadala eti uwe na Mtu mwingine huku na anaekusumbua yupo HUO NDO ULEVI MBAYA😅😅
Kumbuka huyu mpya atajua unae MUME unategemea atakupa PENDO LA DHATI?
Anakupaje pendo la dhati na wewe unae mwingine? Maana yake atakulaghai ili muwe kwenye UHUSIANO pengine nae anazo sababu zake kuingia penzi lako na kwa upande wako akakudatisha huogopi kujikuta NJIA PANDA?
Usijaribu kuyalewesha MAHUSIANO yako kamwe hutakaa ufurahie zaidi utakuwa MHANGA WA MAPENZI kwa watu wawili wala usimuone ambaye ndiye anae takiwa kuwa nawe, Kila mmoja kwa nafasi yake UTAOGOPA KUMUACHA je nini maana ya kulewesha UHUSIANO wako?
MICHEPUKO SIO DEAL👐 Ukiona huwezi kuendelea VUNJA UHUSIANO na kama unaona unaweza BAKI NJIA KUU🙋
Kumiliki watu wawili ni HATARI KWAKO LAKINI PIA NI HATARI KWAO mwisho wako ni mbaya tu, Huna sababu ya MSINGI kuishi kwenye MAHUSIANO YA AINA HIYO Bora kukosa MAHUSIANO ili ukabaki salama, Kuishi kwingi Kuna starehe yake bwana weeee💃💃💃👅
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria😎


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post