USISEME UNAPENDWA WAKATI HUPEWI MUDA KWENYE PENZI LENU

Image may contain: one or more people, people standing and people sitting

Usiseme UNAPENDWA na hupewi muda kwenye penzi lenu🚫 Ukipewa MUDA tarajia kuzoewa maana MAZOEA HUJENGA UPENDO💏
Akikuzoea atamiss kuwa nawe, Akikuzoea atapenda mitoko pamoja nawe, Akikuzoea atakupigia simu na kuku-sms muda wote, Yaani akijenga mazoea kwako ujue NDANI YAKE KUNA PENDO JUU YAKO.
Tambuwa kwamba kinachoumiza kwenye MAPENZI NI MOMENT'S kwani huwezi kutengeneza Moment kama hujapewa muda, Na hawezi kukuzoea kama hukumpa muda, Wala usitegemee UPENDO WAKE KWAKO kama hamkupeana muda, ni rahisi mno PENZI kuvunjika kama HAMKUJENGA MOMENT'S maana yake hukumpa/hakukupa MUDA ina maana HAMKUJENGA MAZOEA💑
Penzi lisolotawaliwa na MUDA limekufa bila wahusika kujua, Pengine MAHITAJI YA KI MWILI ama sababu za ki mahitaji fulani fulani hizo ndizo zinalisukuma penzi bila wahusika kujua, Mwisho wa PENZI la aina hiyo ni KUKOSA MVUTO na hatma ya wawili hao kuja kuachana bila taarifa, Hakuna msingi na mhimili ujengao PENZI kama MUDA maana MUDA ndani yake Mna MAWASILIANO na jilani yake ni MAKUTANO
Ukiona uko na Mtu ambaye hawezi kukupa MUDA wala usisumbuke kuutafuta MUDA kwa Mtu huyo, Muda hutolewa kwa MOYO basi kama hukupewa MUDA tambuwa wazi MOYONI HUKUWEKWA💃💃💃


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post