Usilazimishe kila mtu unayekutana nae kwenye maisha ya MAPENZI awe wako milele⛔

Image may contain: 2 people
Wapo watu wanakuja maishani mwako kukujenga ki akili na ki fikra, Kuna wengine watakuja ili kukufundisha namna ya kuishi na mwenza wako, Wapo wengine watakuwepo ili kukupa mbinu za kumdhibiti mwenza wako ki Mahaba, Kuna wengine kazi yao ni kukuimarisha ki NAFSI ili moyo wako usiishi kwa mateso, Na wengine watakuja kwako kukufanya uijue thamani yako hata kama watakuwa wanapita tu, Kwa hivyo unalo jukumu la kukubaliana na MAJIRA ili uweze kumpata ambaye yeye huyo ATAKUKUTA UMEKOMAA na kuwa mwenye UFAHAMU💪🏽
Uonapo unanyanyasika sana kwenye MAPENZI ujue uko shuleni, Kubali kufundishwa ili baadaye uweze kumuacha Mwalimu aendelee na kufundisha wengine na wewe ukawe mhitimu💃
Inaumiza kuona uliyempenda yeye alikuwa na sababu zake kwako lakini haina maana ndo huwezi kumpata mwingine NOOOO🚫
Ziko nyakati ngumu zimeandikwa kwako lakini kwa IMANI yako Kuna nyakati nzuri zitakuja na utasahau yaliyokuumiza... Kubari kudharulika ili uheshimiwe, Kubali kutupwa ili uokotwe, kubali kutemewa mate ili aje wa kukuosha, Kubali kushushwa thamani ili THAMANI YAKO ISHIKWE NA WAJUAO THAMANI YAKO👌
Sio kila aliyesema NAKUPENDA alimaanisha, Wengine husema ili kukupumbaza lakini nikutie MOYO haimaanishi umeumizwa mara ngapi? Umelia mara ngapi? Umekata tamaa kwingi, Neno moja nimelitaka kwako UMTUMAINIE MUNGU🙏
Hakuna gumu la kumshinda ALLAH👏
Sema AMEN kuwapa FARAJA wanaopitia magumu kwenye MAHUSIANO/NDOA ZAO.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post