USICHANGANYE MAISHA NA MAPENZI🚫

Dramatic portrait of strong young black couple Stock Photo - 33804688
Maisha ni WATOTO, NYUMBA, GARI, MASHAMBA NA VITU VINAVYOTAJWA KAMA MALI... Mapenzi ni STAREHE💃🕺 ndani yake kuna FURAHA NA AMANI. Yote hayo yanatajwa kuwa sehemu ya mahusiano ama ndoa, Ukiona mtu anakuingiza kwenye Mahusiano ama ndoa na wala haongelei usitawi wa mahusiano aliyopo ujue huyo hana malengo nawe, 

Mwenye malengo kabla ya MAPENZI anatakiwa ajadiliane nawe kwa vitendo juu ya MAISHA japo upande huu unahitaji umakini sana kwani KUUZIWA MKUFU BANDIA NI SHERIA... lakini mtu anapokuwa anayo dhamira ya dhati yeye ndiye anatakiwa kuwa mwanzilishi wa kujenga maisha, Maisha utaratibu wake ni UTEKELEZAJI! Ukiona uko kwenye mahusiano ama ndoa na mtu ambaye anategea wewe ndo uwe mwanzilishi wa jambo lihusulo maisha JIONGEZE...

 Ni aibu kubwa kwa mwanaume kumtegea mkewe afanye MAISHA NAE kwa sababu eti yeye ni kichwa cha nyumba, Ndugu yangu hata kondoo anacho kichwa chake, Wewe ukijipa moyo kwa neno la MANABII KWAMBA MUME NI KICHWA CHA NYUMBA na hauwi kama maandiko yanavyotaka ujue UNAJIPA CHEO KISICHOKUHUSU😎

Kichwa gani hata hujui mkeo anavaa size gani ya skate? Kichwa gani mwaka unaisha wala hujawahi kubeba hata kilo moja ya nyama? Kichwa gani hujui hata ada ya mtoto wa kiuno chako? Kichwa gani wewe usiyejua kuwatunza wa nyumbani kwako? Nakuuliza wewe unayejitapa ni MUME na wala hujisumbui kumpenda mkeo, Ndugu yangu kama ulikuwa unatarajia kuoa kwa ajili ya MTEREMKO TARAJIA kula vyakula walivyonunua wanaume wenZio, Wewe si mvivu wa kuhudumia? Wacha ujidanganye kwa kuamini cheti cha NDOA huku mwenzio aliishakutoa moyoni na mwilini AMEKUFANYA KAMA PICHA ILIYOKO KWENYE FLAME🤣🤣


Man rudi kwenye misingi ya kiume wacha kupenda miteremko UNAJISHUSHIA HESHIMA KWA MWANAMKE WAKO🙋🏻‍♂
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria📌


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post