UONGO UNA MWISHO WAKE!!

Image result for MAPENZI YA MBALI; HATAKI UENDE KWAKE ANATAKA AJE YEYE KUKUTEMBELEA.
Wanafunzi watatu wa chuo fulani walinogewa na kusheherekea siku ya weekend, kiasi kwamba wakashindwa kujiandaa na mtihani ambao ungefanyika jumatatu, Wakapanga plan ya kumdanganya mkuu.
Asubuhi wakamuwahia mkuu muda mchache kabla ya mtihani kuanza huku wakiwa wamejipakaza grisi na oili chafu, Wakamwambia hivi "Samahani mkuu, tumeshindwa kujiandaa na mtihani kwa sababu jana tulikuwa kwenye harusi, wakati tunarudi gari ilituharibikia njiani, tukajitahidi kuitengeneza kwa taabu sana, kama utuonavyo tulivyochafuka.
Mkuu akawaelewa na kuwaambia wao watafanya mtihani siku ya jumatano.
Siku ya Jumatano wakaenda kwa Mkuu na kumwambia kuwa wako tayari kwa mtihani maana walikwisha jiandaa tayari.
Mkuu akasema sawa akawaambia kila mtu aingie katika chumba cha mtihani. na kila mmoja akamuweka chumba tofauti.
Aliwaandalia maswali manne (4) tu!
1. Nani alikuwa anaoa ama kuolewa?(marks 25)
2. Ni wapi ambako harusi ilikuwa ikifanyika? (marks 25)
3.Ni wapi ambako gari liliharibikia? (marks 25)
4.Aina gani ya gari ambayo iliharibika? (marks 25)
Nawatakia mtihani mwema.
NENO MOJA KWA MKUU TAFADHALI!!


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post