Tunapofanya maamuzi mabaya au chaguo baya, na tukaona majibu yake kwamba tulikosea Wengi wanakata tamaa na kuingiwa ugomvi usokuwa na mwisho saa zingine kupeana talaka, wanakimbiana, wanapata uchungu na kuondoka kwenye maisha ya ndoa bila kujua sababu hasa ya tatizo lililo mbele yao, Najua kuhusu watu kuishi kwa woga ama kujenga ndoa iliyo na hofu lakini hayo husababishwa na usiri wa tabia za wana ndoa, Badiri makovu yako kuwa FURAHA ili uupe Moyo wako nafasi ya kuendelea mbele, Usiruhusu mabaya yote uliyopitia kukupoteza ama kukuingiza kwenye HASIRA...
Hakuna aliye salama kwenye MAHUSIANO/NDOA kwa asilimia 50, Wengi tunabebeana madhaifu na kusameheana ili siku zisonge, Simaanishi kwa mtu ambaye hataki kujua kwamba yeye ni mzigo ila navumilia laaa hasha kwa mtu ambaye anatambuwa makosa yake, Sisi sote tulishafanya maamuzi mabaya na tunajutia na sisi sote tunaweza kusamehewa na kuanza upya, kikubwa ni kutambuwa KOSA NA KULIACHA LIKUONDOKE ili ufungue ukurasa mpya, Muumba wetu atatusamehe, na atatuonyesha kipi cha kufanya baada ya mateso,
Kama uliisha kosea na ukabaini kosa INUKA UKAMSHUKURU MUNGU KUPATA KIBALI HICHO... Sio wote wanaweza kubaini kwamba MAHUSIANO/NDOA uliyopo ni kirusi kwa maisha yako, Mwambie yeye MUUMBA wako akupe REHEMA ili utoke kwenye kifungo hicho, Mahusiano yanawatesa wengi wala sio wewe peke yako! Ni wakati tu kuruhusu AKILI isimame yenyewe na MOYO ukubari nyakati, Unapolilia UPENDO wa mtu asiyekuwa na UPENDO ni kujitaabisha na mwisho wa maisha na mtu wa aina hiyo ni KUKUACHA UKIWA ULIISHAPOTEZA MUDA, NGUVU, na hata Mali, Yeye aliishi nawe kwa malengo na ametimiza adhima yake anasepa.
#Elista_kasema_ila_sio_she ria
#Elista_kasema_ila_sio_she
Post a Comment