UNATAMANI MKEO AWE KAMA ALIVYO MKE WA JILANI YAKO?

Image may contain: one or more people, people sitting, people eating, table and food
Kwanza nicheke kisukuma🤣🤣🤣🤣
Pole yako kaka! Yaani kufikiria MKEO awe na heshima ndani na nje unawajibika wewe mwenyewe KUMFANYA AWE KAMA UNAVYOHITAJI... Jilani yako humsaidia mkewe kufua, kupasi nguo, kupika, anawapenda watoto wake, harudi nyumbani mikono mitupu, hana ratiba za siri, anampenda mkewe, anawapenda ndugu wa mkewe, anajua hitaji la mkewe kitandani🛌🏻
UNATAKA UFUNDISHWE HAYO ILI UMFANYIE MKEO WAKATI WEWE HUNA MOYO WA KUFANYA HAYO? Labda nikuuulize;
Unahitaji mkeo akutii ama akupende? Maana kama ni mkeo kukupenda FANYA YAMPENDEZAYO! Maana UTII sio sehemu ya UPENDO but palipo na UPENDO KUNA UTII... Kwa sababu ndani ya UPENDO mna heshima na ukiheshimu unakuwa umetii, Mwanamke akifurahi moyo wake hukunjuruka na kuwa mweupe👌
Hapo Babu ni kama kumpiga chura teke kwenye mwelekeo wa maji nini kinafuatia? Mwanamke anahitaji Mwanaume mwenye URAFIKI WA MOYO wala sio kingine, Jifunze kwa makosa yako na sio kujifunza kwa waliofanikiwa maana wenZio waliishavuka kiwango chako, Acha kutamani maisha ya watu bali yatengeneze ya kwako ili yakupe Furaha 🙋🏻‍♂


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post