Nijambo la kawaida kumsikia mtu akilalamika kuwa mpenzi wangu, mume au hata mke wangu huwa hanipigii simu wala kunitumia meseji mara kwa mara, kila wakati nilazima nimuanze mimi, mtu analalamika na kujuiona kama vile hapendwi. Mara nyingi hii hutokea kwa wanawake na inauma sana kama kila siku wewe unakua mtu wa kumtafuta mpenzi wako, anakua hajali na unajiona kama unajipendekeza.
Ulishawahi kuhisi hivyo, sasa wakati mwingine kweli inawezekana hakupendi, anakuchukulia poa kwakua anaona unampenda zaidi. Lakini wakati mwingine sio hivyo, mara nyingi na kwa idadi kubwa ya watu ambao huniomba ushauri kuhusu suala hili tatizo ni kwao hao wanaopiga simu mara kwa mara. Kwamba wewe ambaye unajiona kama unapenda zaidi kuliko mwenza wako ndiyo mwenye tatizo na si huyo unayeona hakujali.
Tatizo kubwa nikuwa humpi muda mpenzi wako wa kukumiss mpaka kukupigia simu. Labda nifafanue kidogo katika maisha ya kawaida watu hupigiana simu wakiwa na shida flani, hasa wanaume, mpaka kuwe na kitu falani ndiyo hupiga simu, mimi binafsi kuna baadhi ya ndugu zangu naweza kukaa mwaka bila kuongea nao, sio kwamba siwapendi hapana lakini sina cha kuongea nao.
Lakini katika mapenzi watu hupigiana simu kwakua wanatamaniana, wamemisiana, unapokaa na kujihisi mpweke unaona njia rahisi ya kupata faraja ni kwa kumpigia simu mpenzi wako. Huwezi kumpigia tu kama hujamkumbuka, kama huna cha kuongea hapana nilazima umkumbuke. Sasa kuna watu ambao hawakupi hata muda wa kuwamiss na kuwakumbuka, kwamba kila wakati anakupigia simu mpaka unamchoka.
Labda twende kwenye mfano huu, asubuhi umeamka mapema kabisa unampigia mpenzi wako simu kumjulia hali, mnasalimiana mnaongea yanaisha, hapa katikati unamtumia meseji mbili tatu anakujibu. Mchana wewe wewe unampigia simu na kumjulia hali, kumuuliza kama kala au la, jioni nako unampigia simu kama katoka kazini au la, usiku kabla ya kulala husubiri hata akupigie unakua na kiherehere unapiga tena.
Sasa ndugu yangu umekua kutwa mara tatu kama dozi ya Malaria unataka yeye akumiss saa ngapi? Naomba uniambie hapo, umempigia simu mara tatu, tena nyingine akiwa kazini ana stress zake halafu unataka akupigie na wewe, inaamaana kwa siku mpigiena mara simu sita! Mnaongea nini hapo? Hivi hana kazi ya kufanya kweli?
Halafu simu zote hizo hakuna hata moja ambayo mnaongea vitu vya maana zaidi ya umeamka, umekula, ushatoka kazini, umelala sijui na nini mpaka unaboa? Unamuona online Whatsapp badala usubiri na wewe umisiwe kiherehere chako ni lazima utume meseji wewe, lazima umuanze tu! Sasa haiishii hapo pamoja na kupiga simu hizo kila mara kama huduma kwa wateja!
Pamoja na kwamba hukua na kitu cha maana ulichokua unamuambia, lakini sasa kama ulimpigia halafu akaacha kupokea, kama ulimtumia meseji hakujibu, wakati akipokea badala ya kumuambia kilichofanya umpigie unaanza kulalamika kwanini hupokei simu zangu, kwanini hujibu SMS zangu, kwanini hivi! Kwanza kama ni mimi nakukatia simu!
Ni ujinga narudia ili mjifunze vizuri ni ujinga eti mtu unampigia simu kapokea halafu unaanza kulalamika kwamba kwanini hapokei simu? Sasa unaongeaje naye kama hapokei? Hapokei kwakua unapiga mara kwa mara na hakuna cha maana unachoongea, hapokei kwakua zimekua nyingi zinamfanya ashindwe kufanya kazi, hapokei kwakua hajakumiss na humpi nafasi ya kukumisss!
Nakuambia hivi kwakua mkeo, mumeo, mpenzi wako au mchumba wako hawezi kukuambia ila niseme kama una tabia hii inaboa. Hembu fanya hivi muache akumiss, mpe nafasi ya kukupigia simu, nataka kama una tabia hii hembu anza kujiwekea kuwa unapiga simu mara moja tu. Kwamba anza kwa kuhesabu kuwa kama nimempigia simu asubuhi mchana apige yeye, kama nimempigia leo kesho apige yeye.
Kwamba ukishampigia mpenzi wako simu, usimpigie tena mpaka akupigie hata ikichukua miezi miwili, hata akikaa wiki hakupigii inamaana hajakumiss. Najua unatamani kupiga kila mara ila jizuie kama kweli unataka awe anakupigia tofauti na hapo utakua ni mtu wa kupiga simu kila siku na kulalamika kuwa hupigiwi kumbe hujampa muda wa kukumiss.
Najua huu ni ugonjwa wa wanawake wengi, wanapiga simu kila mara halafu wanalalmika wao hawapigiwi, sasa akupigie nini wakati kila saa mnaongea, unapiga wewe. Lakini unataka apokee wakati anajua kuwa kila akipokea ni kulalamika tu, mimi nikikupigia au nikipokea simu halafu kazi ni kualalamika tu nakuambia subiri nitakucheki baadaye nakata simu halafu utakuta sipatikani tena, badilika.
MTAGI RAFIKI YAKO AMBAYE KILA SIKU ANAKULALAMIKIA HII ISHU!
Post a Comment