Uliwahi kuona MWENYE CHUKI AKANENEPA?


Image may contain: 2 people, people smiling
Kwani mwenye chuki kutwa akisumbuka na jambo asilolipatia majibu mwisho wake hukonda pasipo kuwa na ufumbuzi, Kuishi na donge moyoni ni kujipa maradhi na muda mwingine dhambi... Ikiwa Mwenzi wako amekukosea ni vyema ukazungumza nae kuliko kukaa nalo moyoni ukidhani ni suruhisho huku ukibaki kununa wakati mwenzio hana Habari na asijue hilo linalokusumbuwa, Hakuna mahusiano yasiyokuwa na magomvi lakini ikiwa kila mmoja akajuwa nafasi yake katika mahusiano ni vyema kumaliza tofauti mapema kuliko kuruhusu zikachukuwa na yale mazuri mwisho wa siku ni kila mmoja kuona hana sababu ya kuendelea, Mahusiano mengi yamekufa kwa wenza kuhesabiana makosa na hilo limekuwa tatizo kubwa, UMOJA siku zote huyaondoa mahesabu ya makosa, UTENGANO husababisha kuhesabu makosa... Ni jukumu la kila mmoja kuijuwa THAMANI ya mwenzi wake kuliko kukata tamaa akipanga kwenda kutafuta mwingine huku akisahau kuwa HAKUNA ALIYE MKAMILIFU lakini aweza kuwa mkamilifu ikiwa hutamkatia tamaa.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post