UJUMBE WA LEO: JE! UNAFIKIRI UMEROGWA AU UNA MKOSI???.... LA HASHA HAYA NDIO MAMBO MAKUU YANAYOKWAMISHA WENGI KUFIKIA MAFANIKIO.


Image result for NDOA SIO UTANI, SOMA STORY HII.
1. Kuwaza mapen-zi, michepuko na ngon* kila wakati :
:ukitaka kufanikiwa kimaisha hauna budi kuruhusu kichwa chako kufikiri mambo ya msingi na kimaendeleo, ukiwa mtu wa kufikiria mapenzi tu na michepuko huwezi kupiga hatua yeyote kimaisha katika kiwango unachotarajia maana utakua unajipotezea mda na fursa nyingi hasa ukizingatia mapenzi yananyonya mda, pesa na akili (uwezo wa kufikiri ya msingi kwa wakati). Maombi na sala kwa Mungu ndio suluhu pekee kuweza kuukomboa wakati na kuifanya akili yako kuumudu mwili na tamaa zake.

2. Kupenda mafanikio ya harakaharaka.
Watu walio wengi wanapenda sana mafanikio ya haraka. Kwa mfano, ukitaka kumpa mtu mpango wa mafanikio na ili akuelewe vizuri na haraka, mpe mpango unaompa uhakika wa kutajirika kesho. Hili ni tatizo kubwa sana linalowakabili watu wengi. Watu wengi wanaishi kwa kutegemea mafanikio ya haraka kitu ambacho ni hatari.

Na ndio maana utakuta watu wanashindwa kujihusisha na shughuli za maana na matokeo yake wanakuwa wapo tayari kutafuta njia nyingi za mkato ili kufikia mafanikio hayo. Haya ndiyo matokeo ya michezo ya bahati nasibu na mingineyo ili kujipatia pesa. Suala la mipango ya maendeleo ya muda mrefu kwa watanzania walio wengi halipo.
Suluhisho.

“Jiwekee mipango na malengo imara ya kukufikisha kwenye mafanikio makubwa, acha kutegemea mafanikio ya haraka utakwama bila ubishi.”

3. Kushabikia mambo.
Kwa Watanzania walio wengi uzoefu unaonyesha wengi wao ni watu wa kushabikia sana mambo ambayo hata yasiyowahusu. Ni tabia ambayo imekuwa ikijengeka siku hadi siku. Sio ajabu sana kwa sasa, kukuta watu wakiongelea jambo fulani kwa muda mrefu kuzungumzia maisha ya watu wengine tena kwa ushabiki mkubwa.

Bila shaka umeshawahi kuona makundi kama haya ambayo mara nyingi yanaongelea mpira, siasa na mambo mengineyo mengi ambayo hayana msaada kwao. Kuongelewa hayo mambo inaweza isiwe mbaya ila iwe kwa kiasi. Vinginevyo utajikuta unapoteza muda wako mwingi kumzungumzia Neymar analipwa kiasi gani na kusahau maisha yako.

Suluhisho.
“Jifunze kuwa shabiki mkubwa wa maisha yako, acha kushabikia maisha ya watu wengine hayatakusaidia.”

4. Kupoteza muda.
Muda ni kitu ambacho hakina thamani kabisa kwa watu wengi. Walio wengi wengi hujikuta wakipoteza muda wao kwa mambo madogo madogo ambayo hata hayana msaada kwao. Huu ni mfumo wa maisha ambao umezoeleka na wamekuwa wakiuishi watu wengi hivi kwa mazoea na imekuwa kama utamaduni.

Mara nyingi sio ajabu sana kusikia mtu akikwambia ngoja niende mjini nikapoteze muda. Maanake mtu huyo yeye anajiona ana muda mwingi kiasi cha kwamba anao mwingine wa kupoteza. Kwa maisha haya ya kuishi kupoteza muda ambao ungetumika kukupa mafanikio, kama utayaendeleza uwe na uhakika itakuwa ni ngumu sana kwako kufanikiwa.

Suluhisho.
“Usipoteze muda wako hata dakika moja kwa mambo yasiyo ya msingi, tumia muda wako kwa mambo ya mafanikio, utakuwa mshindi na utafika mbali sana kimafanikio”
SOMA; Je, Unachotaka Kufanya Umekubaliana Nacho Ndani Yako? Soma Hapa Kujua Zaidi.

5. Kuishi bila malengo.
Kwa bahati mbaya pia watu walio wengi wana tatizo la kuishi maisha yasiyo na malengo maalum. Hapa hata ubishe vipi huu ndio ukweli. Wengi hujikuta wakiwa na malengo ya mdomoni ambayo siyo ya kuandikika na matokeo yake baada ya muda mfupi hujikuta wamesahu hayo malengo yao na kurudia maisha yao ya awali.

Bila kujiwekea malengo utajikuta unaishi maisha yaleyale. Maisha ya kuishi tu ilimradi kuna kucha na kukosa mwelekeo maalumu. Ukiona unaishi maisha hayo, elewa kabisa kuwa huna mafanikio. Kukosa malengo, hicho ndicho kitu kinachowaangusha wengi katika harakati za kufikia mafanikio makubwa.

6. Kujiona una mikosi.
Fikra nyingi za wengi wanafikiri hawafanikiwi kwa sababu wana mikosi. Hayo ndiyo mawazo yao. Kwa kadri wanavyozidi kuamini hivyo, ndivyo ambavyo huzidi kufanya mambo mengi kwa mkabala huohuo wa kimkosi na kujikuta hawafaniiwi kufika popote. Ni mawazo hayahaya ambayo wengi wetu wanayo kila kukicha na yanawaangusha.

Kwa maisha kama haya , hupelekea maisha ya wengi kwa mabaya siku hadi siku. Ni vyema kuwa makini na mawazo na maisha uliyonayo kwa ujumla ili uweze kufanikiwa.

Nakutakia SIKU Njema Mungu Akubariki na kukulinda


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post