Ni kwa jinsi gani ulishawahi kutafakari ROLLS ROYCE au BENTLEY hazina matangazo?
SABABU:
Wanajua thamani ya bidhaa yao ndo inawaletea wateja.
SOMO:
Ukiitambua thamani yako, hauitaji kuomba watu wakupende, kuwa wenza wako, kutumia mda na wewe au kukupenda.
Jiamini jinsi ulivyo, Kila mtu anaweza kukuchukulia anavyoweza kwa mtazamo wake, Kuna ambao watakuona HUFAI lakini itakuwa kwa wakati huo ambao wao hawaoni THAMANI YAKO
Kuna ambaye ataijua THAMANI YAKO lakini hayupo tayari kukuonyesha ama kwa wivu au kwa KUTOJIAMINI KWAKE
Fikiria zaidi KUJI-BLAND kulingana na ulivyo, Wala usijaribu kuruhusu Mtu akuone sio kitu pengine kwa sababu ya VIJI-MSAADA alikupatia, Pengine uliyomsaidia yeye ni YENYE IMPACT kubwa.
Bin adam wanahesabu UKUBWA WA MSAADA KUWA NI PESA lakini hawajui neno liponyalo MOYO hilo lina gharama kubwa,
Ndo Maana pesa inabaki kusimama kwenye MAHITAJI YA KI AKILI lakini isiweze kupambana na MAHITAJI YA NAFSI.
Usiitangaze THAMANI YAKO uwe na hakika UBORA HUO HUO MDOGO UTAMLETA AMBAYE ATAIJUA THAMANI YAKO.
Kujiamini kunawaondosha mbele yako wasokutakia mema pamoja na wanaokushusha, Fikiria zaidi USHINDI kuliko KUSHINDWA😎
#Elista_Kasema_ila_Sio_She
Post a Comment