SOMO: UKOMBOZI WA NDOA


Ndoa ndio msingi wa familia na mafanikio yote ulimwenguni kwa kuwa Mungu huonekana huko. Mungu ameweka uumbaji wake kwenye ndoa. Alitangaza hukumu na msamaha wa kwanza kwenye ndoa. Muujiza wa kwanza wa Bwana Yesu aliofanya hadharani ulikuwa kwenye harusi ya Kana ya Galilaya. Hivyo basi, kusudi la Mungu hutimia kwenye ndoa inapokuwa nzuri. Ndio maana adui huwinda sana ndoa ili aweze kuiharibu.
Ndoa uhitaji ukombozi na uponyaji kwa kuwa ndiko penye majeraha mengi ya moyoni yanayoweza kuleta uharibifu na maangamizi kwa wanandoa na ndoa yenyewe. Uponyaji huu ni vyema kufanyika hata kabla ya kuingia kwenye ndoa maana kila mmoja hutokea kwenye mazingira yake. Mazingira hayo huathiri tabia na maisha ya mhusika kiroho na kimwili.
Tofauti za wanandoa husababisha maumivu mengi na huchangia kwa sehemu kubwa kuvunjika kwa ndoa na kuharibika kwa watoto pia. Si vema kwa wanandoa kuendelea kubeba desturi mbaya za kwao kwa sababu ni lazima zitawagharimu.
Moyo uliojeruhiwa hupoteza upendo na shauku kwa mwingine. Katika hali hii panahitajika juhudi kubwa kurejesha pendo lililopotea kwa mwanandoa. Uponyaji wa moyo unapofanyika, amani hurejea na kusababisha mafanikio kwenye ndoa. Hivyo basi ni vyema kila mmoja atoke kwao na kwa pamoja waanze jambo jipya.
Wanandoa wengi huteseka na kufa mapema kwa sababu ya ujinga wa kuoana kwa tamaa zao na sio kwa mpango na mapenzi ya Mungu. Wengine hufanya hivyo kwa kutafuta urahisi wa maisha na baadae huwa katika majuto makubwa. Hata wale walio katika kusudi la Mungu hawafahamu namna ya kulinda ndoa kupitia Neno.
Kila kitu mtu anachotafuta ili awe bora kipo ndani yake na siyo cha kubahatisha. Hii ni pamoja na mwenza, familia, mali, elimu na mengineyo. Vitu vyote hivi haviwezi kuonekana kwa sababu vimefichwa ndani yako. Ili viweze kuonekana vinahitaji Neno, jukumu lako ni kujua namna ya kuomba ili Mungu akufunulie. Akishafunua, ng'ang'ania hayo maono yako; naye Mungu akiona hivyo, hata kama yalikuwa mbali kiasi gani huyasogeza kwako.
I do love Efatha❤️❤️


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post