SOMA HISTORIA HII PENGINE UTAPONA!

Image may contain: 1 person, outdoor
Maisha si tu kula🍔 kuvaa👗👔 kusoma👨🏻‍🎓👩🏻‍🎓 kujenga nyumba🏘 kumiliki Gari🚗 BALI MAISHA NI KUWA NA AFYA NJEMA... Huwezi kuimarika ki afya kama una tatizo la mawazo yaliyojenga akilini mwako na moyo wako kuvunjika kwa hayo unapitia, Kaka Elista mimi ni Mwanamke kama unavyonitazama, Kwa ujumla nina kila haiba ya mapenzi, nina mvutia kila Mwanaume, nimejaaliwa mali, Elimu, lakini sina AMANI WALA SINA FURAHA! Nimekuwa na safari ya muda mrefu nikiitafuta AMANI PAMOJA NA FURAHA lakini kila nililojaribu kulifanya ili nipate Amani nilipoteza muda pamoja na nguvu zangu, Kuna wakati ulifika nikafanya ukarabati wa nyumba yangu kwa kuweka mazingira mazuri ikiwemo na kubadili SAMANI ZA NDANI LAKINI NILIPOLALA USIKU MAWAZO YALIJIRUDIA YALE YALE YANAYONITESA... Kuna wakati nilikwenda GYM kufanya upembuzi yakinifu walau nimuone mwanaume anayelingana na hitaji langu wala sikudumu nae mwisho kabisa nilirejea kwenye mateso pamoja na kujiona nina mikosi, Wanaume nilowahi kutembea nao wala hawakunipenda kwa sababu Mimi sikuwaonyesha UPENDO kutokana na wingi wa stress, Nimekutana na Madaktari bingwa wakaniandikia vipimo lakini majibu ni kwamba Mimi ni mzima, Nilikutana na Ma-counsellor nao kila mmoja alijitahidi kuniondoa katika hali ile lakini muda tu nilikuwa nikiteseka tena, Elista ni mengi nimepitia na sasa niseme kwamba NIMEKATA TAMAAA YA KUISHI NADHANI SIWEZI KUFURAHIA WALA KUWA NA AMANI TENA KWENYE MAISHA YANGU😭
Pole sana Dadaangu, Nasikia uchungu mwingi juu ya historia yako but Samahani ninalo swali moja kwako "MPAKA HAPO ULIISHABAINI KINACHOKUTESA?"
Elista niseme ninalo jibu dogo kwako "MIMI NILIKUWA NA MWANAUME WANGU TULIPENDANA SANA ILA BAADAYE AKAGUNDUWA NILIKUWA NINA MAWASILIANO NA BABA WA WATOTO WANGU KITU AMBACHO KILIMUUMA NA KUMVUNJA MOYO KWANI MIMI NILIMJENGA KWENYE MLENGO WA SINA MAWASILIANO NA MZAZI MWENZANGU" Duh😳
Dada hilo ndilo kosa lako dada, Ulikosa msimamo ndo maana ukaamua kusafiri na wanaume wawili kwa wakati mmoja, Pole sana, Dadaangu ULIPOTEZA AMANI NA FURAHA YAKO Kwa uzembe kabisa, Yule ni mzazi mwenzio na mliisha achana lakini yako mambo mnawasiliana kuhusu watoto IKO MIPAKA ULITAKIWA KUIJENGA KWANI KAMA NI ADA ALIPASHWA AKALIPE SHULE, NI MAHITAJI YA WANAE MNGEWAFUNGULIA AKAUNTI WATOTO PESA ZA MAHITAJI ZIKAPITA HUKO na Mengine mengi yanayofanana na hayo ili tu kulinusuru penzi lako ambalo wewe mwenyewe unalipenda, Nikwambie kitu? X wanatabia ya kujishusha wanapohisi wameachwa na wanataka kurudi, Ni kweli kabisa umezaa nae na pengine anawapenda wanae Kwani unaishi nao hivyo anawasiliana nawe juu ya matunzo ya wanae JE UNAJUA ANAWAZA NINI JUU YAKO WAKATI ALIKWISHA FAHAMU HUMPENDI TENA? Wahenga waliposema MOYO WA MTU NI CHAKA WALIMAANISHA... Umeharibu misingi ya AMANI yako kwa kujidanganya mwenyewe, Nikupe siri ya wanaume;
Hakuna Mwanaume atajua Mwanamke wake ana shiriki ki mwili na Mwanaume mwingine na akaendelea kukupenda, Anaweza kuendelea kuwepo kwako lakini asiwe na upendo nawe ila kwa sababu zake akaendelea kuvumilia, Kama ulivyosema mwenyewe SIO KWA MALI WALA PESA ukitafuta kuwa na AMANI lakini yote ni UBATILI! UPENDO WA DHATI hautafutwi bali mwenye nao huja kwa bahati sana na watu wenye UPENDO WA DHATI NI WAVUMILIVU SANA ila akiishakinai huondoka wala asirudi, Ushauri wangu UNAWEZA KUMPATA UKAONGEA NAE? Elista nimeishafanya kila namna ya ushawishi lakini imekuwa NOTHING😭
Sipendwi tena wala hataki kunipa nafasi japo anisikilize, Nahitaji mawazo yako Kaka.
Pole tena dadaangu Kwani nakuona kabisa vile unahangaika ukijaribu kureja AMANI NA FURAHA YAKO japo naamini kabisa ULIIPOTEZA BAHATI YAKO... Wazo langu la mwisho JARIBU KUTAFUTA MTU AMBAYE YUPO KARIBU NA HUYO ALIYE NA FUNGUO ZA AMANI YAKO vinginevyo utataabika sana, Kosa lako uliudanganya moyo wako ukidhani utapata mbadala wa huyo mwanaume, UPENDO WA KWELI NI WA MTU MMOJA TU haijalishi umeoa ama kuolewa unaweza kuishi na ambaye si wa PENDO LAKO na wakati ukiwadia akaja ambaye ametajwa na PENDO LAKO UTAJUA KUPITIA MOYO, MWILI NA AKILI ndo maana leo unateseka dadaangu, Basi tena Sina ushauri katika hilo fanya juhudi kumrejesha yule ambaye anatajwa na MOYO WAKO!
Asante sana kaka ushauri wako nitaufanyia kazi, Nimeamini kabisa UPENDO NI WA MTU MMOJA mwingine hana nafasi.

Maana halisi ya ujumbe huu ni;
Ukigunduwa unampenda mtu hakikisha usikubari akakuondoka maishani mwako, Unaweza kuwa unapitia changamoto za hapa na pale lakini ni BORA AWEPO KUILINDA AMANI NA FURAHA YAKO! Kuliko kukubari akuondoke na wakati ukijua yeye ndiye umpendaye, Epuka kumtafuta wa kuziba gape la mtu ambaye ulimpenda maana sio kila mtu anaweza kulingana na mwingine, Ni heri kulinda mwovu asikupokonye kuliko kusubiri upokonywe n then ukitafute ulichopoteza... MAJI YAKIISHA MWAGIKA HAYAZOLEKI usingoje Maji yamwagike bali hakikisha unalinda yasimwagike.
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria💪🏽


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post