Sio kila Mwanaume anaweza kumsababisha Mwanamke awe na nuru na muonekano mzuri,

Image may contain: 2 people, people smiling, close-up

Vivyo hivyo sio kila Mwanamke anaweza kumsababisha mwanaume awe na nuru pamoja na Muonekano mzuri, Maana katika UPENDO kuna uhitaji wa NAFSI na hapo ndipo paliposababisha wawili KUHITAJIANA... Hakuna kazi ngumu kwenye maisha ya Mapenzi kama MTU KUMPA MWENZA WAKE FURAHA! Wengi huishi kwenye mahusiano ama ndoa kwa mazoea na kutunza heshima kwenye jamii huku mioyo yao imejaa madonda ambayo hayawezi kuponywa wala kutibiwa maana aliyesabisha hajui kama ameumiza moyo wa mwenza wake, Kukosea sio kosa maana ni kujisahihisha, Kosa ni kurudia kosa kwa sababu ni makusudi kutokana na ukweli kwamba MTU ALIISHA AMBIWA AMA KUONYWA lakini bado anarudia kosa lile lile... Mtu asiyejuwa kutuliza MOYO wa mwenza wake huyo hajajipanga kumpa mwenza wake FURAHA! Huwezi kusema niko kwenye Mahusiano ama ndoa wakati ndani ya moyo wako umejawa huzuni na simanzi pamoja na woga ulojawa kukata tamaaa, Usiishi maisha ya MAPENZI kwa kutarajia maana MOYO wa mtu ni siri iliyo na giza, Kadiri unavyoweza kutarajia ndivyo ambavyo unazidi kuwekeza MUDA, AKILI, MWILI wako mwisho wa siku uje kujutia, Tabia ya mtu ni kama NGOZI unaweza kuibadili lakini haitakosa mabaka, Mateso ya MAPENZI hayana masaidizi ila ni wewe unayekabiliana na changamoto hiyo, Utetee MOYO wako kwa uhalisia wala usiwe kama unasikiliza mziki kwamba utapoza maumivu kwa faraja ya nyimbo, Usiombe kukutana na Mtu ambaye anayo masrahi yake binafsi kwako, Mapenzi yanataka UHALISIA na sio picha.
#Elista_kasema_ila_sio_sheria ðŸ’ª


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post