SIMULIZI; JINSI MKE WANGU ALIVYONIACHA KWASABABU YA SALAMU!

unhappy african man having a fight with wife in bedroom Stock Photo - 21587969
Nimeachana na mke wangu wa ndoa ya miaka 15 kwasababu siku moja niliamua kumtoa out, ilikua ni sherehe ya kikazi. Mara nyingi mimi si mtu wa kwenda hizi sherehe lakini ya siku hiyo ilikua ni lazima niende, nilipandishwa cheo na kuwa mtu mkubwa. Basi nikaema ni lazima niende na mke wangu, nampenda na ana wivu sna ahivyo nilijua kuwa kama nikienda peke yangu nikachelewa kurudi basi kelele zake zilikua za mwezi mzima kama si mwaka kabisa.
Basi akajiandaa tukaenda, mambo yalikua mazuri mpaka Binti mmoja ambaye ni secretary wangu alipokuja kutusalimia, ilikua ni baada ya sherehe, nilisimama mimi na mke wangu pamoja na jamaa yangu mmoja hivi. Yule binti akaja akanisalimia, nikaitika, akamsalimia na huyo jamaa mwingine kisha akamuambia mke wangu “Habari yako Dada… akamalizia umependeza…” Akaongea ongea maneno mawili matatu kisha akaondoka.
Sherehe ikaisha tukaondoka huku nikimshukuru Mungu mambo yameenda salama, lakini njiani mke wangu kanuna, nikasema hapana simsemeshi kwani nilikua nimechoka sana kujibizana naye. kufika nyumbani anaanza kulalamika.
“Inamaana umenitoa out ili kunionyesha malaya wako?” Nikajua kimenuka, nikaanza kuwaza ni Malaya yupi ambaye nimemuonyesha mke wangu mpaka akanuna hivi. Nikaanza kuwaza kuanzia mwanzo wa sherehe mpaka mwisho, nilikua makini sana kusalimiana na watu, hata kuhsika mkono nilikua sishiki mdada kwakua namjua mke wangul, nilikua makini sana na macho yangu, akipita mwanamke ambaye najua kamzidi mke wangu hata kwa ukucha tu basi naangalia pembeni au najifanya kununa.
“Malaya gani tena huyo?” Nikaamua kuuliza kwani niliwaza nakuwazua mpaka nikachoka. Ndiyo akaanza kunifungukia, yule binti ambaye alikuja kutusalimia mwishoni alinisalimia mimi na rafiki yangu halafu yeye akamuambia habari.
“Yule ni mwanamme wako, yaani kaja kabisa kunichora, najua ulimuambia kabisa kuwa nitakuja, kwanini akusalimia wewe na mimi ananiambia za saa hizi, inamaana haniheshimua na wewe ndiyo unampa kiburi! Halfu eti anajifanya kunisifia, kwa kupendeza gani, nguo yenyewe hii ya mwaka jana, haipo hata kwenye fasheni, unaona alivyokua amependeza, lile tako lote anakuja kunichora kuwa nimependeza!”
Mke wangua liongea mpaka akakaukiwa mate, nikajielezea, nikaomba misamaha, nikaongea mpaka nikahcoka nikalala. Nimelala bado analalaimika kuwa namhdarau ndiyo maana nalala simsikilizi. Asubihi naamka si kama kawaida, hajaniandalia chochote, namuuliza akaniambia kuwa muambie yule Malaya wako akakuandalie, si ndiyo mke wako wa kazini unamuona wa maana sana, si ulienda kunionyeshea! Basi nikasema isiwe shida, nikanyoosha nguo zangu, nikavaa na kuondoka, siku hiyo hatukuenda kazini pamoja, aligoma yeye akaenda kivyake ofisini kwake.
Nikajua yameisha, kumbe kaana kumfuatilia yule dada, kaingia Instagram yake, akaona picha mbili, moja nilipiga naye wakati wa chakula, tena tulikua wengi ila shida mimi ndiyo nilikaa naye, na nyingine Binti lipiga selfie ofisini kwangu. Mimi hata sikuijua, lakini ni secretary wangu, anaingia ofisini kwangu nikiwa sipo sasa mimi nitaanza kufuatilia kwenye mitandao kuona kuwa anafanya nini/ basi ikawa ugomvi kuwa kanizoea mpaka haheshimu ofisi yangu. ikawa sihida, akaniambia kuwa kachoka, aani kachoka visa vyangu hivyo anataka kuondoka.
Nilijua utani, ila usiku akanaimbia kuwa nichague kati ya yeye na yule binti, mimi nikamuambia kuwa nimechagua yeye, kumbe sikumuelewa, alitaka nimfukuze yule binti kazi au yeye aondoke.
“Hivi huyu mwanamke ana akili kweli, anadhani kuwa Bosi ni kama kuwa Admin wa Group la Whatsapp kwamba mtu akikuudhi tu unamuondoa!” Nikawaza, sikumuambia, nikamuelewesha kuwa kampuni si yangu, mimi ni bosi tu lakini siwezi kufukuza. Aligoma kuelewa, ikanibidi niseme isiwe shida, nikafanya yakufanya nikamhamishia yule binti ofisi nyingine nikatafuta mwingine.
Lakini haikusaidia, alichokua anataka ni binti kufukuzwa kazi kwani yeye kufanya kazi na mimi inamnyima amani. Nikasema huu ni ujinga, ameniendesha sana katika miaka yote huyo ya ndoa nilikua sijawahi kuchepuka hata mara moja, si kwakua sikutani na vishawishi, hapana, lakini siko hivyo tu, mimi ni mwanaume wa mwanamke mmoja, yaani nikipenda napenda, kama nikichepuka basi ni kesho nakamatwa kwani nahamia jumla jumla. Nilishajaribu kipindi niko chuo, nilikua na mtu wangu nikachepuka ila nikawa siwezi kubalance tena.
Lakini pia nilikua nimeapa kuwa wanangu hawatelelewa na Baba wa kambo hivyo kila siku nilikua mtu wa kujishusha, mke wangu akiongea kidogo naomba msamaha yanaisha, akikohoa mimi najamba, yaani nilishazoea, nilikua bize, nakaguliwa sana hivyo nikaona kwanini kujipa mawazo. Sasa mke anataka nimfukuze binti wa watu kisa tu binti kamuambia habari badala ya shikamoo. Haikua sawa kabisa, lakini hata kama ningetaka, mimi ni bosi si mfalume, kumfukuza mtu ni lazima kuwe na sababu la sivyo hata mimi hiyo kazi nakua sina.
Basi nikamuambia hapana, haiwezekani, nikakomaa na hicho, akawa ni mtu wa kupiga simu, kulalamika kwa ndugu, wazazi wake, nikaitwa mpaka kwa Mchungaji kuwa namsaliti na mfanyakazi mwenzangu na sitaki kumfukuza kazi. Mwaka mzima tunasumbuana, hakuna amani, amekazania kuwa nimfukuze au niache kazi ili kuwe na amani, nikasem hiki ni kitu gani, nikaa kimya. Siku moja narudi nyumbani nakuta nyumba tupu, kaondoka, ameenda kupangisha sehemu, anasema kuwa hawezi kuishi na mimi hivyo anataka talaka na watoto kachukua.
Niliona kama kioja, lakini wiki ilipita, mwezi, nikaiota ndugu basi akasema nichague kati ya huyo binti na yeye, nimfukuze kazi kama kweli sitembei naye au nimuache. Nikafikiria sana mpaka nikashindwa, nikaamua kumtafutia yule binti kazi sehemu nyingine, niliona si sawa kumfukuza na kwakua ilishajulikana kuwa mke wangu hamtaki basi nikimfukuza itakua shida, nikaamua kuhangaika, nikahonga na kuhonga mpaka ikapatikana nafasi tena sehemu nzuri zaidi, nikajua hapa binti hachomoi, nikamuambia kuwa kuna nafasi sehemu falani omba.
Basi binti kweli akilinganisha msahara ni zaidi ya mara mbili, akiangalia na usalama wa ajira akaomba, akapata na kuanza kazi. Nikamuambia mke wangu kuwa nimemuondoa yule binti sifanyi naye kazi, basi akarudi, lakini hakukaa hata wiki mbili, anakuja ananiambia kuwa anataka talaka, kaanza mchakato kabisa. Namuuliza kwanini mbona binti nimemuondoa, ananiambia;
“Mnaniona mimi mjinga, yaani umemtoa hapo umeenda kumtafutia kazi sehemu nyingine, analipwa msahara mkubwa kuliko hata aliokua analipwa mwanzo! Tena umeenda kuhonga kabisa ilia pate hiyo kazi, hapana, najua ni mipango yenu, badala ya kumpa dahabu unampa zawadi ya kazi, kwataarifa yako na mimi nina watu, jinsi ulivyokua unahangaika uili ajairiwe ni kama ni mke wako, mbona mimi hujawahi kunihangaikia hivy?”
Nilishiwa pozi, ghafla nikaitwa baraza la kata, mke wangu safari hii hakuondoka, alikua anadai talaka hivyo mimi nikaambiwa niondoke yeye abaki na watoto. Kusema kweli nilishachoka kuomba msamaha, sikutaa suluhu tena, aliposema anachotaka ni talaka, hataki kuendelea kuwa na mimi nilimuambia;
“Hata mimi nimechoka, kama hicho ndiyo kitu unachotaka basi hakuna hata haja ya kurudi kanisani, waambie wakupa barua mimi nipo tayari, kama ni mali hata ukitaka kuchukua zote chukua, sihitaji kitu chochote.” Niliongea kwa hasira, nilishakata tamaa kweli, mke wangu alijua kuwa ni utani lakini niliamua, akapewa barua, akaenda mahakamani, akapata na wakili na kuanza habari sijui za kugawana mali.
“Sihitaji chochote, achukue kila kitu ila ninachohitaji ni amani tu. Nimegundua kuwa siwezi kuwa na furaha nikiwa na huyu mwanamke, achukue kila kitu, niliwaambia.” Mpaka hukumu inasomwa, mke wangu anachukua talaka hakuamini, alijua kuwa nitabadilika mwishoni, alichukua kwa kejeli, ndugu zake wakanitukana, wakaongea mambo mengi sana lakini sikujali tena. Nilishaamua kuwa sibembelezi tena. Basi kila mmoja akashika lake, baada ya kuachana basi nilianza maisha yangu, nikaenda nyumba ya kazini ambayo napewa kutokana na cheo changu nikamuachia nyumba na kila kitu.
Nikawa na amani, wanangu nahudumia, ada nalipa mimi, chakula na kila kitu. Kwa mwezi nilikua nampa mpaka milioni moja kwaajilia ya matumizi huku ada na mahitaji mengine nikitoa mimi. Nilikaa kwa amani kwa miezi sita, yaani nilikua na furaha mpaka nikajiuliza hivi kwanini nilioa kama maisha ni raha hivi. Lakini kumbe mke wangu hakua na amani, nashangaa naitwa Ustawi wa jamii kuwa nimetelekeza watoto sihudumii. Akalalamika sana, uzuri pesa nilikua namuwekea kwenye akaunti yake au za dharura natuma kwa M-Pesa.
Basi nikamuacha akaenda kuongea mpaka akachoka, alipomaliza nikatoa risiti, nikaweka mezani, waliokua wanamsikiliza walishangaa kwani nilitoa risidi za ada shuleni, slip za Benki na kila kitu. Akaishiwa pozi, akaanza kusema hataki hiki hataki kile, wakamtolea uvivu na kumuambia huwezi kuweka mashariti yoyote, hela unayopewa ni nyingi na kuhusu watoto anaruhusiwa kuwaona wkaati wowote akitaka. Tukaondoka, kanuna, ananitumia meseji eti nimehonga ili wampendelee, sikujali, nikaamua kuendelea na maisha yangu.
Miezi sita baadaye kwa maana ya wiki iliyopita basi naitwa kanisani, nakutana na Mama yake, Mchungaji na mke wangu, wanataka tuogee. Mke wangu anataka turudiane kwajaili ya watoto, mchungaji ananiambia ndoa ya Kanisani haivunjiki hata kwa amri ya mahakama, Mama yake ananiambia watoto wanateseka. Mimi nikawaangalia wote, nikawaambia kuwa mimi nina furaha, aliniacha yeye, sikumuacha hivyo kanifungulia mlengo mwingine wa furaha ambao siwezi kuufunga tena, nikaondoka, naendelea na maisha yangu. inawezekana na mimi nilikua na makosa kama binadamu lakini kwakua sasa hivi nina furaha basi sitageuka nyuma, maisha yanaenda nashukuru Mungu kwa hilo, nina amani mpaka najionea wivu.
MWISHO


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post