#SipendagiUjingaMimi
Hizi ni tabia zinazokera sana za matumizi ya simu za mkononi na kila mmoja wetu anapaswa kuziacha:
1. Upigaji wa selfie za ovyo au picha za uchi na kuzipakia mtandaoni kisha ku TAG watu wenye heshima zao na wengine waume au wake za watu SIO TABIA NZURI, ACHA INABOA MNO. Tabia hii wanayo zaidi wadada hususani wa mjini.
2. Ukinipigia simu mara moja sijapokea, nitumie ujumbe nikiwa huru nitakupigia, acha kuendelea kunipigia simu lukuki kama vile kuna nyumba inaungua, unakimbiza mgojwa hospitalini au unanidai.
3. Kama umenipigia simu na sina namba yako, acha kususa/kununa, huwezi jua ni kwa sababu gani sina namba yako (simu mpya, simu ilifuta namba zote n.k), jiamini!
4. Ukinipigia simu nina haki ya kupokea na kutokupokea, mimi sio mtumwa wa simu yangu, hivyo acha kukasirika kwa vile sikupokea simu yako.
5.Na pia ukiniandikia msg nikapata taarifa tayari, sio lazima nikujibu, labda kama ni lazima natakiwa kufanya hivyo, acha kumaindi mambo madogo hivyo!
6. Ukiniadd kwenye What'sApp group bila kutaka idhini yangu nitatoka tu, acha kunitafutia kesi kuwa ninaringa, nina haki ya kuruhusu taarifa gani naruhusu zinifikie kwenye maisha yangu na zipi sizihitaji au si za maana kwangu.
7. Wewe ukiwa mtu wa kubeep tu kila siku nitakublock, inakuwaje shida ya kuongea nami ni yako lakini gharama ya kukusikiliza ni yangu?
8. Walioweka tafadhali nipigie waliwalenga wale watu wenye dharura/shida ukweli, haiwezekani wewe kila siku unanitumia tu tafadhali nipigie, ni lini utapiga?
9.Tafadhali ukiwa kwenye basi linaloenda mbali, pokea simu na zungumza kwa sauti ya chini na kwa ufupi, sio kila mtu anafurahishwa na masimulizi yako njia nzima.
10. Sasa wewe uko sinema na unapokea simu na unazungumza kwa nguvu hivyo ukirushiwa popcorn utamlaumu mtu kweli?
11. Uko kanisani, msikitini au kwenye mkutano, watu wanasikiliza mambo ya maana halafu simu yako inaita kwa sauti na nyimbo za ajabu, halafu bila aibu unapokea kweli? Au unaanza kusumbua watu kutoka nje - focus!
12. Unapokea simu yako sehemu ya watu wengi na unazungumza kwa sauti kubwa kama una kipaza sauti tumboni, hivi unafahamu kuwa simu ina kipaza sauti tayari kwa hiyo ukizungumza taratibu bado utasikika?
13. Uko msibani, watu wanaomboleza, wewe unapokea simu na kuanza kuzungumza juu ya mtoko wako wa jana, hivi una akili kweli?
14. Nimekupatia lifti kwenye gari yangu na tunaenda mbali, basi unaanza kupiga simu moja baada ya nyingine na kunifanya mimi kusikiliza story zako ambazo sizihitaji, kuwa makini, utajikuta unatembea kwa mguu ndugu!
15. Umeomba muda wangu tukutane , na badala ya kuzungumza nami kila baada ya dakika moja vidole vyako viko kwenye simu, mbona tunapotezeana muda rafiki, si unyanyuke na uende huko unakotaka kwenda?
Nitaishia hapa kwa sasa, mwenye kero yake juu ya matumizi mabaya ya simu niliyoisahau aongeze. Tuwe wastaarabu wandugu.
#Imepenya haijapenyaaaaa??!!!.....
Kama imepenya SHARE NA MARAFIKI ZAKO WAIPATE
Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda
Post a Comment