Maumivu ya MOYO mtu unajipa mwenyewe kulingana na vile wewe mwenyewe unashindwa kubalance UHITAJI WAKO MWENYEWE🙇
Unaweza kuwa mhitaji wa KITU ama MTU lakini wewe Mwenyewe hujajua namna nzuri ya kupokea UHITAJI WAKO.
Kama unahitaji KITU lazima ujue una uwezo nacho? Maana mbuzi🐐 anakula kwa urefu wa kamba yake, Kama unamhitaji MTU je una hakika kwamba yupo upande wako? Maana unaweza kumhitaji mtu awe wako wakati huo huo ANA MWINGINE ukabaki kuwa MHANGA😇
Wahenga wa kizungu walipata kunena;
"IN FOLLOWING YOUR HEART MAKE SURE YOU ARE READING ON THE SAME PAGE WITH YOUR PARTNER"
Muda mwingine unaweza kujua kwamba uko kwenye UHUSIANO SALAMA na kumbe wewe ni kivuli🌳 cha mwingine, kwamba umekuwepo ili kuondosha ukali wa MATATIZO YA MTU.
Upendo wenye KUMAANISHWA HUITOWESHA AIBU lakini ukiona upo kwa MIPAKA ujue wewe ni MWAMVULI🌂 TU nyakati za JUA☂ ama MVUA☔ kumbuka wakati wa jioni🌇 HUNA THAMANI TENA.
Huwezi kutaka kujua kama UNAPENDWA AMA HUPENDWI kwa MANENO MATAMU bali ni rahisi kujua ikiwa HUPENDWI au UNAPENDWA kwa MATENDO 💑
Aliyekupenda anajua kukufanya ujue ANAKUPENDA💏
Post a Comment