SAMAHANI KAKA, TAYARI NINA MTU"=HILO NDIO JIBU KUNTU LINALOWAINGIZA CHAKA WANAWAKE WENGI BILA KUJUA

Image may contain: 1 person
Haina maana kuwa ukijihami kuwa tayari una mtu ndio itasaidia wewe kumpata mtu sahihi na mwenye mapenzi ya kweli bali huenda ikawa njia rahisi zaidi ya wewe kumpata mtu tapeli, kicheche na laghai wa mapenzi, ambae atakusababishia maumivu makali mwishowe uishie kusema WANAUME WOTE MBWA TU.

Jamaa kakufuata kaanza kukubembeleza kuwa anakupenda na angependa uwe wake nawe kwa ufupi ukamjibu, "SAMAHANI KAKA, NINA MTU". Jamaa hakukata tamaa akatumia juhudi na skills zake zote jumlisha uongo mwingi na mbwembwe mwishowe binti ukalegeza msimamo na hatimaye kukubali.

😅TAFAKARI SASA
Hivi unafikiri kama alijua una mtu na bado akaamua kukomaa na wewe hadi akakupata unafikiri amepata uzoefu gani?
😁
Mtu wa namna hiyo nkupe tu siri kiufupi mara nyingi huwa ni KICHECHE MNO yaani yeye suala la wewe kuwa katika mahusiano na mtu mwingine yeye hajali ndio maana anatupa karata yake ivo ivo, sawa ni kweli huenda ni mbinu yako kumpima mwanaume kama kweli anakupenda ila hakika kwa jibu hilo la NINA MTU utaishia kuchezewa.

Mtu wa namna hiyo dada yangu hata ukimpata mkaoana usijifariji kuwa umepata mume bali tambua aeza kuja watafuna shemeji zake, majirani, housegirl, mashost zako na hata ndugu zako wa karibu maana yeye ni mzoefu wa kupangua hoja ya SAMAHANI, NINA MTU.

😁 Wanaume wengi wastaarabu hueshimu mno mahusiano au ndoa za watu, hawapendi kuthubutu japo kuonja mali ya mtu ukiwajibu tu kuwa TAYARI UPO KWENYE MAHUSIANO wanaacha kukufuatilia na wanakuheshimu kama mke wa mtu, ila wanaume vicheche wao hawajali siku hizi husema HAINAGA USHEMEJI TUNAKULA.

Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda

Usisahau ku LIKE


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post