Wanaume wengi wanasumbuliwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, hali inayo afanya washindwe kufurahia tendo la ndoa na wenzi wao wa kike. Hizi ni baadhi ya sababu zinazo sababisha upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume.
1. Msongo wa akili.
2. Ulevi kupita kiasi.
3.Kupooza kwa mwili
4. Presha na ugonjwa wa kisukari.
5.Wasiwasi wa kutekeleza tendo la ndoa
6. Uoga wa kufanya tendo la ndoa.
7.Uzoefu wa kukatisha tamaa wa siku za nyumaa
8. Mazingira yasiyoridhisha wakati wa tendo la ndoa.
TIBA (HUWEZA KUWASAIDIA HATA WANAWAKE)
1. MLONGE/ NAZI. Chukua nusu kikombe cha maua ya mlonge, ongeza kijiko kimoja cha chai cha vumbi la machicha ya nazi. Chemsha katika nusu lita ya maji kwa muda wa dakika 15, kutengeneza aina ya supu. Chuja na baada ya kupoa kila jioni kunywa nusu glasi, saa moja kabla ya kwenda kulala. Endelea na tiba hii kwa muda wa mwezi mmoja.
2. KITUNGUU MAJI/ASALI. Ponda ponda kitunguu maji cheupe cha ukubwa wa kati ( gramu 50) . Kaanga ndani ya mafuta ya samli, baada ya kupoa changanya na kijiko kimoja cha mezani cha asali. Kula nusu saa kabla ya kwenda kulala. Endelea na tiba kwa muda wa mwezi mmoja.
3. ZABIBU NYEUSI ( BLACK RAISINS ). Chukua zabibu kavu nyeusi. Zioshe vizuri na maji ya moto. Kula gramu 40 za zabibu ikifuatiwa na glasi moja ya maziwa. Fanya hivyo mara tatu kwa siku. Endelea na tiba kwa muda wa mwezi mmoja.
4. TANGAWIZI/ ASALI. Chukua nusu kijiko cha chai cha juisi (au unga) ya tangawizi. Changanya vizuri na kijiko kimoja cha mezani cha asali. Tumia pamoja na nusu yai lililochemshwa kila jioni kabla ya kwenda kulala. Endelea na tiba kwa muda wa mwezi mmoja.
5. KAROTI. Saga au pondaponda gramu 200 za karoti. Ongeza nusu ya yai lililochemshwa na kijiko kimoja cha mezani cha asali. Changanya kwa pamoja. Kula nusu saa kabla kwenda kulala . Endelea na tiba kwa muda wa mwezi mmoja.
6. BAMIA/ ASPARAGASI. Chukua gramu kumi za unga wa mizizi ya bamia. Changanya na gramu 15 za unga wa mizizi ya asparagasi Chemsha katika glasi moja ya maziwa kwa muda wa dakika tano. Kunywa asubuhi na jioni saa moja kabla ya kwenda kulala. Endelea na tiba hii kwa mwezi mmoja.
Hii ni tiba rahisi ya vyakula kwa wale ambao wana tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ama kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa (kwa wanawake) na hawana uwezo wa kununua dawa inayo tibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume
Post a Comment