Nazungumza na wewe ndugu yangu.
Unapoanzisha mahusiano, ni vyema ukatambua kuwa mahusiano ni suala la kujitoa wewe pamoja na vile ulivyonavyo kwaajili ya yule umpendae.
Chochote utakacho kitoa au utakavyo jitoa kwaajili ya mpenzi wako, amini kuwa ni kwaajili tu ya kulijenga penzi lenu.
Lakini isikufanye uamini kuwa ndicho kitamfanya awe nawe milele, big NO.
Lakini isikufanye uamini kuwa ndicho kitamfanya awe nawe milele, big NO.
Nimeshuhudia watu wengi leo hii wameshindwa kumove on tangu waachwe na wale waliowapenda.
Wanashindwa kufurahia maisha yao, wanaishi maisha ya masikitiko na majuto tangu waachwe.
Wanashindwa kufurahia maisha yao, wanaishi maisha ya masikitiko na majuto tangu waachwe.
Kwasababu moja tu "Nilikuwa nampa kila kitu alichoniomba, nimemnunulia hiki na kile, nimepambana nae kutoka zero mpaka 100, kala pesa zangu sana, tangu nilale nae ndio kaniacha".
Narudia tena, chochote utakachofanya, utakachotoa, kwaajili ya mpenzi wako.
Fanya tu kwaajili ya kulijenga penzi lenu, lakini kamwe isikae akilini mwako kuwa ndio itafanya asikuache.
Fanya tu kwaajili ya kulijenga penzi lenu, lakini kamwe isikae akilini mwako kuwa ndio itafanya asikuache.
NB: Binadamu wachache sana ndio wanaweza kukumbuka na kuthamini mema•mazuri uliyowahi kuwafanyia.
Hivyo unapotoa kitu au kujitoa wewe mwenyewe, toa kwa moyo mmoja.
Na wala usiweke matarajio makubwa, ili hata siku mkiachana isibaki majuto kwako.
Hivyo unapotoa kitu au kujitoa wewe mwenyewe, toa kwa moyo mmoja.
Na wala usiweke matarajio makubwa, ili hata siku mkiachana isibaki majuto kwako.
Post a Comment