Nakuuliza Mwanaume NI NANI ALIKUFUNDISHA MBINU YA KUMPATA MKEO?

Image may contain: 1 person, standing
Najua huna jibu la kutamka but ndani ya nafsi yako unalo jibu kwamba ULIVUTIWA NAE HATA KAMA NI KWA TAMAA AMA UPENDO HATA ULIPANGA AWE WAKO... Sasa rafiki kilichokupata ni kipi baada ya kumpata na kumuweka kwenye himaya yako FURAHA yake ya awali umeitowesha na sasa UNAMLIZA?
Ni kweli kabisa UPENDO ukiisha huwezi kujua mwenzio anatesekaje juu yako, Lakini Kwanini ulimuingiza kwenye DHAMANA YA MOYO🤷🏽‍♂
Maana kama usingemuingiza kwenye kukupenda naamini hata yeye asingeumia, Kosa liko wapi mpaka anateseka hivyo? Najua hana kosa ila ni vile MATUMIZI YAKE YA KUTUMIKA KWAKO YAMEISHA Yaani kwa lugha nzuri ame-expire huna shida nae tena, Umekinai si ndiyo? Basi mwache aende usimuwekee vikwazo huku ukijuwa huna shida nae, Ni wivu wa mali kwamba akiondoka atakupunguzia mlivyochuma pamoja? Ni wivu kwamba hutaki akapate mwingine? Ama ni vile umemfanya kijakazi wako unahofia mazoea alokuzoesha utayakosa? Kama ndivyo Kwanini sasa hutaki kumpa AMANI?
Mwanamke by nature haishi kwa MAFANIKIO YA MALI AMA VITU bali wameumbwa kuishi kwa FURAHA💃
Sasa wewe kama unaona mafanikio yako ndo siraha ya kumtesea Mwanamke nakwambia kwamba UMEBUGI! Mwanamke kuyaanza maisha bila kitu kwake sio issue, issue ni kwamba UPENDO WAKE UPO KWAKO TU... Najua wanaume wengi wakijua Wanapendwa hujisahau na kuishi na wake zao kwa manyanyaso eti wakijidai HANA PA KWENDA maana aliisha mkongoroa na kumpausha🙈
Ni udhaifu wa wanawake wengi kudhani hawezi kuvutia tena, but ngoja nikwambie Mwanamke KILA SHETANI NA MBUYU🌳 wake, Ukitaka kujua kwamba wewe thamani yako ni kuitwa Mwanamke HEBU NENDA KAOGE, PAKA MAFUTA MAZURI, VAA NGUO INAYO ONYESHA UBORA WAKO N THEN TEMBEA KUTOKEA NYUMBANI KWAKO UMBALI WA KAMA KILOMITA 1 TU uje unipe majibu hapa😂
Wacha kukaa unalialia tuuuu na wakati Uko na kitu cha GHARAMA NDANI YAKO! Ukitaka kujijua wewe ni wa tofauti hebu jiulize Kwanini MTU AKIWA ANAKUTAKA KWA MARA YA KWANZA HUKUBEMBELEZA KWA GHARAMA ZOTE? Muda mwingine we nae unaharibu unakuwa mdhaifu sana kiasi jamaa anakuzoea, Hebu usiishi na Mwanaume akakuzoea uone ulivyo wa THAMANI wallah atakuona mpya kila siku, usikubari Mwanaume akuone wa kawaida KILA SIKU ITENGENEZE THAMANI YAKO ili uwe Brand isiyopitwa na wakati💪🏽
Napenda AMANI yako lakini pia UKIFURAHI nafarijika🙋🏻‍♂


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post