Wanaume wengi hususani wa kabila lile fulani(silitaji) kwao kumpiga mwanamke hufikiri ndio dawa pekee ya kumdhibiti ndani ya ndoa na kumfanya awe na heshima, La hasha hapo ndugu zangu wanapotea mno kwa kuwa mapenzi ni hisia zinazopaliliwa kwa furaha, upendo, amani na undugu ila sio mangumi, mapanga, mateke na tindikali. Uvumilivu wa wanawake katika ndoa zao pamoja na machungu yote wanayopitia ikiwemo kunyanyasika unatokana na mioyo yao ambayo daima imetawaliwa na mapenzi ya dhati hivyo anahitaji tu mwanaume utambue nafasi yako na kumtendea haki stahiki hakika haitohitajika fimbo, ngumi, panga, hirizi, pesa nyingi, magari, juju, uchawi au kipigo ili kumdhibiti.
mwanamke anapokua katika mahusiano na mwanaume ambaye anampenda sana, yaani yule ambaye yuko moyoni achana na wale ambao wapo kwenye wallet kuna maswali ambayo huwa hayakomi...
Huwa anajiuliza;
"Hivi ananipenda kweli kama ninavyompenda? Kwanini kanichagua mimi? Mbona sina kalio kama flani...hapendi makalio kweli? Mhh! Hajamtamani rafiki yangu kweli? Walivyokuwa wanaangaliana mhhh! Namuachia mungu..."
Kwa kifupi kichwa chake kitazungukwa na maswali mengi ya kwanini yeye na si wengine. Nikazi yako wewe mwanaume kumkumbusha kwanini unampenda na njia bora ya kumuambia si kwa kusema nakupenda kwakuwa umweupe...Itamuumiza pale atakapokuona upo na mweupe zaidi yake.
Mshike mkono akiwa katikati ya marafiki zake, toka naye pembeni kidogo kama mnajificha vile kisha mshike kiuno vizuri ukimvuta kwako...yaani ile kinguvu mpaka auhisi msisimko wa mwili wako (najua mshaelewa) kisha muambie nakupenda...Akiuliza kwa nini muambie kwa sababu ni wewe.
Msifie tabasamu lake, wakati akiwaza kudhani labda ndicho ulichompendea msifie mahco yake, kabla hata hajawaza nini cha kusema sogea mbali kidogo kisha muite, akija akikuuliza unasemaje muambia ..."Hata unafikiri kuna kitu...nilitaka tu nikuone unavyotembea moyo wangu ufurahi..yaaniiii..."
Mfanyie surprise ya zawadi mbali mbali mara kwa mara hakika utazidi kuuteka moyo wake, sio lazima ziwe zawadi za gharama bali mwanamke huwa na tabia ya kutafsiri kwa huruma na hisia pale unapompa zawadi, hujijibu "duh Kaka wa watu ananijali kweli kweli, hakika ananipenda sana, nkimsaliti ntamuumiza mno, bora nitulie na huyu tu, asante Mungu kwa kunipa huyu anaenijali hivi"
Mpende uliye nae, mjali mkeo, mpendezeshe, mthamini, huyo ndiye malaika wako usitazame kwingine bali mtimizie yote kumbuka KAZI SIO KUMUOA, KAZI NI KUMTUNZA ADUMU KATIKA VIWANGO VYA UBORA ULIOMKUTA NAVYO TOKA AKIWA KWAO.
Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda
Post a Comment